Unga wa ngano, nyama, maziwa, mayai, viazi vyachangia kuongezeka mfumuko wa bei

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

MFUMUKO wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Septemba 2021 umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka 3.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2021.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi wa Sensa za Watu na Takwimu za Jamii Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja amesema, hilo ni badiliko la asilimia 0.2 ikilinganishwa na nchi jirani kama Kenya na Uganda.

Amesema kuwa, Septemba 2021 umeongezeka kwa asilimia 0.3 kwa kila moja kukiwa na maana kuwa kuongezeka huko kunaashiria kasi ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo Agosti, mwaka huu.

Amesema, kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Septemba 2021 kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei wa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa mwezi Septemba, 2021 ikilinganishwa na mwezi Septemba 2020.

"Kwa baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei ni pamoja na unga wa ngano 6.8, nyama ya ng’ombe 3.4, maziwa ya unga 9.2, mayai 5.0 na viazi mviringo 4.7," amesema Minja.

Kwa upande mwingine amesema, baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfuko wa bei ni pamoja na gesi ya kupikia kwa asilimia 2.7, mkaa kwa asilimia 3.5 na huduma ya malazi kwenye nyumba za kulala wageni kwa asilimia 5.7.

Hata hivyo, amesema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Septemba 2021 wa asilimia 4.0 bado upo ndani ya lengo la Serikali la muda mfupi na wakati wa kuwa na mfumuko wa asilimia 5 ambao unawezesha shughuli za kiuchumi kufanyika bila athari, na kwamba serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto zinazofanyia bei na huduma kupanda.

Kwa upande wa nchini Kenya mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 6.91 kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba 2021 kutoka asilimia 6.57 kwa mwezi Agosti 2021 huku nchi ya Uganda ukiongezeka hadi asilimia 2.2 kutoka asilimia 1.9.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news