UVCCM Kinondoni yawafunda vijana

Na Anneth Kagenda

VIJANA nchini wameaswa kuendelea kumuenzi Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan.

Sambamba na kuchukua hatua madhubuti za kujikinga kwa kwenda kupata chanjo ya UVIKO-19.
Pia imeekezwa kuwa ni vyema vijana hao wakaendelea kutii nasaha na maelekezo yanayotolewa na viongozi wao kuanzia ngazi ya chini hadi ya kitaifa na kwenda kuyafanyia kazi na si kuyapuuza.

Wito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam na Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Kinondoni, Ally Simba wakati akimkaribisha mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama na Maadili UVCCM Makao Makuu, David Jonh Malecela wakati wa semina kubwa na ya aina yake iliyotolewa kwa vijana hao iliyohusu ulinzi na usalama lengo likiwa kuendelea kumuenzi mwalimu.

Katibu Simba alisema kuwa katika kumbukumbu ya Baba wa Taifa Oktoba 14, 2021 pamoja na kuendelea kumuunga mkono Rais Samia wameona upo umuhimu wa kuwapa vijana semina hiyo ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha majukumu yao kwenye Taifa pamoja na kutii maagizo yanayotolewa na viongozi wao na kwenda kuyafanyia kazi.

Mgeni rasmi Malecela, akizungumza kwenye semina hiyo, aliwaasa vijana hao kuzingatia mafunzo na maelekezo waliyopewa na wakufunzi pamoja na viongozi wao akiwemo Katibu Simba huku akiwataka kwenda kuyafanyia kazi kwa lengo la kuilinda Nchi yao.

"Semina hii mliyopewa, mafunzo pamoja na hamasa naomba mkavifanyie kazi,lakini pia msisahau kusikiliza maelekezo yanayotolewa na viongozi wa Kitaifa ikiwemo kwenda kuchanja na pia mkitoka hapa naomba mwende kuwa mabalozi wazuri kwenye mitaa yenu kwani ni wajibu wa vijana kuendelea kuweka ulinzi katika Mitaa kwa Ulinzi Shirikishi,"alisema mgeni huyo.

Alisema tangu miaka ya 1967 wakati wa Tanu hadi sasa na yale yote aliyokuwa akiyahimiza Mwalimu hakuna kilichobadilika sana na kwamba kazi zake nyingi zimeendelea kuhasisiwa jambo linaloonekana kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa na maono ya mbali na kwamba kwa kipindi chote hicho vijana wapo salama.

"Kwa mantiki hiyo basi vijana Nchi mzima, bodaboda, Machingawa hawana budi kuendelea kuyalinda na kuyafanya yali yaliyohasisiwa na Marais wetu wote akiwemo Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Hayati Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete, Hayati Jonh Magufuli huku wakiendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ili kukiweka chama Salama,"alisema Malecela.

Diwani wa Mabwe Pande kupitia CCM, Muhajirina Obama aliwapongeza viongozi na watoa mada za Ulinzi na Usalama na kusema kuwa ni muda muhafaka kwa vijana kuchukua maelekezo hayo na kwenda kuyafanyia kazi na si kwenda kukaa nayo majumbani badala yake utekelezaji uanze mara moja.

"Lakini kitu kingine ambacho ningependa kuwaasa vijana ni kwamba nyie ndio Taifa la leo na la kesho, hivyo hamna budi kuendelea kuyatii maelekezo yanayotolewa na viongozi wenu ambayo kwa asilimia zote ni ya ujenzi wa Nchi yetu," alisema Diwani Obama.

Hata hivyo Diwani huyo aliwaomba viongozi kujitahidi kuwatengea maeneo ya kufanyia shughuli au kutafutiwa viwanda vidogo lakini vizuri na vyenye mwonekano kulingana na shughuli zao "mfano vijana wangu wa machinga zaidi ya miatatu tayari nimewatengea maeneo na eneo hilo linawatosha kwa ujasiliamali na wenye nyumba wamekubali kulipwa na kuondoka ili tuweze kuwapa eneo machinga.

Semina ya vijana hao ya Ulinzi na Usalama ilifanyika Oktoba 14, 2021 katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Wilaya ya Kinondoni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news