Wizara ya Kilimo yapania kukuza kilimo hai nchini

Na Doreen Aloyce,Diramakini Blog

Naibu Waziri wa Kilimo nchini ,Mhe. Hussein Bashe amesema kuwa Wizara ya Kilimo itaanzisha kitengo maalum ndani ya wizara kitakachohusika na kilimo hai ili kukuza na kuendeleza kilimo hicho hapa nchini.

Aidha, wizara kwa kushirikiana na wadau wa kilimo nchini, wataanzisha pia benki ya mbegu kwa lengo la kuendelea kuhifadhi mbegu mbalimbali za asili zitakazomsaidia mkulima kutekeleza kilimo hai chenye tija.
Akiwa mgeni rasmi katika kongamano la kilimo hai lililowakutanisha wadau wa kilimo kutoka maeneo mbalimbali lililofanyika mjini Dodoma, Mhe. Bashe amesema kuwa wizara itaanzisha benki ya mbegu kwa lengo la kuendelea kuhifadhi mbegu za asili zitakazomsaidia mkulima kutekeleza kilimo hai cha uhakika.

"Sisi kama Wizara ya Kilimo, tunaliweka katika muelekeo na kuwa ni senta tutaweka kitengo ndani ya wizara ambapo sasa hivi tuna dawati tu, lakini tutaweka kitengo maalum ambacho kitahusika na kilimo hai, lakini sisi kama nchi ni lazima tuanze mchakato wa kuhifadhi na kusafisha na mbegu za asili ili ziwe zinapatika kwa wingi na kwa ajili ya wakulima kurudi shambani, kwani tusipokuwa makini bàada ya miaka michache tunaweza tujajikuta tumepoteza kabisa mbegu za asili,"amesema Bashe.

Katika hatua nyingine amesema kuwa kuna baadhi ya maduka wanauza mbegu aina za highbreed, lakini huwezi kukuta duka linauza mbengu za asili kwa sababu hazipatikani, hivyo amesema ili viweze kupatikana kwa wingi ni lazima zizalishwe kwa wingi.

Ameendelea kusema kuwa, wizara imewekeza zaidi ya bilioni 10 kwa ajili ya kuendeleza kilimo hai hapa nchini.

"Sisi kama wizara katika nchi hii ni lazima tuanze mchakato wa kuanzisha benki kubwa ambayo itakuwa kwa ajili ya kusafisha mbegu,kuzalisha mbegu za asili ili ziweze kupatikana kwa wingi kwa ajili ya wakulima wetu,"amesema Bashe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news