NA GODFREY NNKO
ANDRIY Mykolayovych Shevchenko mwenye umri wa miaka 45 na raia wa Ukraine ambaye ni fowadi wa zamani wa AC Milan na Chelsea ameingia mkataba wa kuifundisha klabu ya Genoa C.F.C.
Genoa C.F.C ambao wanashiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A) wameingia mkataba na Andriy ambao utadumu hadi mwaka 2024.
Ujio wake unajaza pengo la Davide Ballardini aliyefutwa kazi na Genoa C.F.C mwezi Novemba 6, 2021.
Andriy Mykolayovych Shevchenko aliongoza timu ya taifa ya Ukraine kutinga robo fainali za Euro 2020 ambapo walichakazwa na Uingereza 4-0 mjini Roma, Italia. Aidha, alijiuzulu Agosti 2021, wiki chache baada ya mtanange wa Euro 2020 kukamilika rasmi.
Andriy Mykolayovych Shevchenko alipokuwa akitoa maelekezo kwa timu yake ya Ukraine katika mtanange wa kutinga robo fainali Euro 2020 dhidi ya Uingereza. (Picha na Robert Perry /Getty Images).
Tags
Michezo