BAKITA yatoa onyo vituo vya kufundisha Kiswahili kwa wageni

NA HADIJA BAGASHA

BARAZA la Kiswahili la Taifa Tanzania (BAKITA) limesema kwamba vitendo vya uendeshaji vituo vya kufundisha Kiswahili kwa wageni nchini ambavyo havijasajiliwa na Serikali ni kinyume cha sheria na kanuni za baraza hilo, hivyo hawatasita kuvichukulia hatua ikiwemo kuvifungia.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahi Tanzania (BAKITA), Consolata Mushi wakati wa mkutano wa BAKITA na wadau wa vituo vinavyofundisha Kiswahili kwa wageni nchini uliofanyika mjini Tanga.

Mkutano huo unatokana wa kwanza unajumuisha wamiliki wa vituo na wadau wa vituo vya Kiswahili kwa wageni unatokana na kanuni na sheria za Bakita.

Amesema, Tanzania kuna vituo 15 vya kufundisha Kiswahili, lakini wanajua vipo zaidi ya hivyo, hivyo wanapaswa kutambua kwamba kama wataendesha mafunzo bila kusajiliwa na baraza ni kosa hivyo hawatasita kufungia vituo hivyo.

Amesema, wao kama baraza hawataki kufika huko ndio maana wanatoa wito wakutane wajadili na kusajili vituo kutokana na kwamba wanaposema wanadhibiti ufundishaji wa kuswahili Tanzania ni kuhakikisha walimu wanaotumiwa kufundisha lugha ya Kiswahili wanauwezo wa kufundisha.

Amesema, pia wawe na uhakika wa kufundisha na kila mtu kama alivyobainisha hapo mwanzoni huku akisisitiza kwa kutumia fursa hiyo kuwataka watu wenye vituo vya kufundisha Kiswahili na havijasaliwa waende baraza la kiswahii wakasajiliwe vituo vyao.

“Na sio kwamba tunasema waende wakajisajili ni kwa mujibu wa kanuni na sheria za baraza hilo kwani sababu huwezi kufanya jambo ilihali utambuliki na baraza na kwani bakita ni chombo cha sheria hivyo ukisajiliwa huko unatambuliwa na serikali kama mtu ambayo unakituo ambacho kinatoa mafunzo ya Kiswahili Tanzania,"amesema Kaimu Katibu huyo.

Amesema kwamba, wanaona Kiswahili kinapiga hatua kubwa ambazo si za kawaida waswahili wanasema kimepiga kunako siku maalumu kila mwaka Julai 7 imethibitishwa na Shirika la Unesco kunamaanisha Kiswahili kwa sasa ni lugha inayoheshimika duniani na imebeba dhamana kubwa.
“Kiswahili kimebeba dhamana kubwa kama unavyojua kulikuwa na dhamana kubwa ya lugha sita zilizokuwa zimetengewa siku maalumu duniani, Kiingereza, Kichina, Kifarasa, Kiarabu, Kihispania, Kirusi,”amesema Kaimu Katibu huyo.

Awali akizungumza katika mkutano huo kutoka Shirika la Urithi wa Utamaduni wa Kiswahili (SUUKI) Tanga, Mwalimu Ramadhani Kasimu amesema mkutano huo wa wadau wote wanaofundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni na wao washiriki wenyeji ni muhimu sana kwao kutokana na kwamba sasa kiswahili ni tunu iliyopewa heshima kubwa sio Tanzania bali mpaka nje ya nchi.

Hata hivyo aliishauri jamii kwa sababu kimeshakuwa tunu wakitumie Kiswahili kwao kwenye nyanja mbalimbali kiwape manufaa yenye tija na wakithamini ili kiweza kuwasaidia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news