Bei ya mafuta ya Dizeli yapaa Zanzibar, Petroli, mafuta ya taa mambo safi

NA GODFREY NNKO

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza mabadiliko ya bei za mafuta ambazo zimeanza kutumka rasmi leo Novemba 9, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Uhusiano cha ZURA bei hizo zimepangwa kwa kuzingatia mambo mbalimbali.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta duniani (plants quatations) katika mwezi Oktoba, 2021 kwa lengo la kupata kianzio cha kufanyia mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Novemba, 2021.

"Pia tunazingatia gharama za uingizaji wa mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam, thamani ya shilingi ya Tanzania kwa dola za Kimarekani, gharama za usafiri, bima na premium hadi Zanzibar, kodi za Serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja,"imefafanua taarifa hiyo ya ZURA.

Kwa mujibu wa zura mafuta ya petroli ambayo mwezi Oktoba, 2021 yalikuwa yanauzwa kwa shilingi 2,300 kwa lita mwezi huu wa Novemba, 2021 bei imebakia hiyo hiyo sawa na asilimia sufuri ya ongezeko huku kukiwa hakuna tofauti.

Pia mafuta ya Dizeli kulingana na taarifa hiyo iliyoonwa na DIRAMAKINI BLOG kwa mwezi Oktoba, 2021 lita moja ilikuwa inauzwa kwa shilingi 2,245 na kwa mwezi huu wa Novemba, 2021 lita moja imepanda hadi shilingi 2,265 huku ongezeko likiwa ni asilimia 0.79 ambapo tofauti na mwezi uliopita ni shilingi 16.99.

Aidha, upande wa mafuta ya taa kwa mwezi Oktoba, 2021 lita moja ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi 1,721 ambapo kwa mwezi huu wa Novemba, 2021 yameshuka hadi shilingi 1,686 kwa lita sawa na asilimia -2.06 huku tofauti na mwezi uliopita ikiwa ni shilingi -35.50.

ZURA imebainisha kuwa, bei za bidhaa za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa katika mwezi huu wa Novemba, 2021 zimeongezeka kutokana na kubadilika kwa wastani wa bei za uuzaji wa bidhaa hizo katika Soko la Dunia pamoja na soko la ndani kwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

"ZURA inapenda kuwajulisha wananchi kuwa bei zilizotangazwa ndio bei halali zitakazoanza kutumika kuanzia Siku ya Jumanne (leo) ya Novemba 9, 2021,"imeongeza taarifa hiyo ambayo DIRAMAKINI BLOG ina nakala yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news