CCM yafanya uteuzi wa wa makatibu wa mikoa 32, makatibu wa wilaya 168 TAZAMA majina yote hapa

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuendelea kufanya mageuzi ya kiuongozi na kiutendaji ili kukidhi mahitaji ya wakati, mwenendo wa mabadiliko ya siasa za dunia na madhumuni ya Chama chetu katika kuwatumikia wananchi kikamilifu.
Hivyo Chama kimefanya uteuzi wa makatibu wa mikoa 32, waliobaki vituo vyao vya kazi ni 10, waliopangiwa vituo vipya ni 12 na wapya ni 9; aidha makatibu wa wilaya ni 168 ambapo waliopangiwa vituo vipya ni 67, waliobaki kwenye vituo vyao vya kazi ni 45 na wapya ni 56. Katika uteuzi huu kwa kuzingatia suala la jinsia wanawake ni 67 sawa na asilimia 33.5 na wanaume ni 133 sawa na asilimia 66.5.

Katika uteuzi huu hakuna hata mmoja aliyetoka nje ya mfumo wa Chama Cha Mapinduzi. Makatibu wapya wa Mikoa na Wilaya wametokana na kupandishwa hadhi kwa makatibu wa CCM wa Wilaya, makatibu wa jumuiya za CCM Wilaya na Mikoa, Maafisa wa Chama na jumuiya Makao Makuu kwa utendaji kazi wao mzuri pamoja na makatibu waliorejeshwa kwenye utumishi kutokana na utiifu wao kwa Chama.

Katika uteuzi huu Kamati kuu ya Halmashauri kuu ilizingatia sifa za ziada ikiwemo uadilifu, uaminifu, weledi, uwezo, bidii, ubunifu, jinsia na rika. Makatibu wapya na waliohamishwa vituo vya kazi kwa Mikoa na Wilaya wanatakiwa kuripoti vituo vyao vya kazi mara baada ya kupokea barua zao. Uteuzi wa Makatibu wa CCM Mikoa na Wilaya uliofanyika ni kama ifuatavyo:-

Uteuzi huu umeanza mara moja kuanzia tarehe 6 Novemba, 2021.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,
Itikadi na Uenezi.
8 Novemba,2021

Miongoni mwa makatibu wa hao ni pamoja na Mussa matoroka (Arusha),Adam Ngalawa( (Dar Es Salaam), Pili Mbanga(Dodoma), Mwanamasudi Pazi (Rukwa),Naomi Kapambala (Manyara)

Omar Mtuwa (Katavi), Rukia Mkindu (Iringa),Innocent Nanzabar(Simiyu),Elias Mpanda(Morogoro),Marco Mbanga (Kaskazini Pemba),Alhaji Saad Kusilawe(Mbeya),Donald Etamya Magesa (Shinyanga), Langael Akyoo (Mara),Alexandrina Katabi (Geita),Suleiman Mzee (Tanga), Mobutu Malima (Kigoma).

Wengine ni Julius Peter (Mwanza), Christopher Palangyo (Kagera), Mgeni Musa Haji (Mtwara),Lucy Shee (Singida), Solomon Kasaba (Tabora),Jonathan Mabihya (Kilimanjaro),Mullar Othuman Zuber ( Magharibi), Mohamed Ally Khalfan (Kusini Pemba), Shaibu Akwilombe (Ruvuma), Amina Imbo (Kusini Unguja), Abdullar Mwinyi Hassan (Njombe) Salum Suleiman (Wete Mjini) Juma Mpeli (Songwe), Yusuf Said Goha (Pwani),Barnabas Essau (Lindi) na Ramadhan Rajab Kapeto (Kaskazini Unguja).

Makatibu waliochaguliwa wa wilaya kwa Mkoa wa Arusha ,Kataba Sukuru (Arusha Mjini), Shaban Mrisho (Karatu),Safina Alfred (Monduli),Aboubakar Ghaty (Ngorongoro), Mwadawa Maulid (Arumeru) Gulisha Mfanga ( Meru) na Alaw Haidary (Longido). Kwa kituo cha Dar es Salaam Idd Mkowa (Ilala) Kitte Mfilinge (Temeke),James Mgego( Kinondoni),David Mollel (Kigamboni) na Henry Msunga (Ubungo).















Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news