CHONGOLO: KAZI YA SIASA SIO UONGO, SIO MAJUNGU SIO FITINA WALA SIO UMBEA

NA MARY MARGWE

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kuendekeza uongo, fitina, majungu, umbea na kusingiziana ambapo amewataka kutambua kuwa kazi ya siasa ni kusemeana mema, kupendana, kushikamana na kuneneana mema.

Hayo amebainisha jana katika muendelezo wa ziara yake na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoa wa Kagera akiwa wilayani Muleba kwenye kikao cha shina namba 5 Tawi la Lulanda.

Chongolo alisema, kazi ya siasa sio uongo, kazi ya siasa sio majungu, sio fitina, kazi ya siasa sio umbea na wala kazi ya siasa sio kusingiziana, Kazi ya siasa ni kuombeana mema, kazi ya siasa ni kupendana, kushikamana, kazi ya siasa ni kuneneana mema na wenzio na si vinginevyo.
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kufuatia kupokea taarifa ya viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo walionza kusemana vibaya na kujengeana fitina ikiwa ni maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa ndani ya Chama na jumuia zake mapema mwakani.

"Kazi ya sasa sio uongo, kazi ya siasa majungu, kazi ya siasa sio fitna, kazi ya sisa sio umbea, kazi ya siasa kusingiziana, kazi ya siasa ni kuombeana mema, kazi ya siasa ni kupendana, kazi ya siasa ni kushikamana, kazi ya siasa ni kuwanenea mema wenzio, mkineneana mema mambo yananyooka, mkikaa kutunga yule mbona kasimama na yule yaani mmmh pale kuna ndoa, wewe inakuhusu nini, nawe katengeneze kwani nani kakuzuia kutengeneza yako, na ndoa inaanza kwa kusimama si ndio, kujadiliana si ndio, baadaye inaenda mchakato unakua mchakato baadaye inakua mchakato CCM Oyeee," alisema Chongolo.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu huyo amezitaka Serikali za m Mikoa na Wilaya zinazopakana na ziwa victoria kuendeleza jitihada za kupambana na uvuvi haramu katika ziwa hilo ili kuendelea kufanya hivyo ni kupoteza mapato ya serikali

Chongolo alifafanua kuwa, madhara ya uvuvi haramu katika ziwa hilo ni makubwa na kwamba serikali ikiacha kudhibiti matendo hayo, uvuvi haramu utaendelea kutengeneza mianya ya mazingira magumu kwa mikoa hiyo na wananchi kunufaika na uchumi unaotokana na ziwa hilo.

“Ndugu zangu nataka niwaambie Ziwa Victoria ni uchumi mzuri ambao ukilelewa vizuri kwa kufuata uvuvi unaofuta sheria na taratibu, utasaidia kudumu kwa uchumi ambao unatokana na ziwa hilo miaka na miaka,” alisema Chongolo.

Hata hivyo kwa nyakati tofauti wananchi, Madiwani na Wabunge wa Muleba wakiwa katika ziara hiyo, wameendelea kutoa shukrani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali kwa kuwapelekea fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa yote ya sekondari wilaya ya Muleba na ujenzi wa vituo vya Afya unaoendelea hivi sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news