NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Chriss Mugalu ambaye ni mshambuliaji wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC amerudi nchini kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mshambuliaji huo amerudi nyumbani kwa ajili ya kujiuguza huku akisema atarudi akiwa imara zaidi hapo baadae, Mungu akimjalia afya njema.
Mugalu alipata majeraha wakati Simba SC ikiwa kwenye maandalizi ya kucheza dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana mwezi uliopita ambapo hajarejea uwanjani tangu wakati huo.
Amesema, amelazimika kurudi nyumbani kwao ili apate muda wa kupumzika na kuendelea na tiba zaidi.
“Bado sijafahamu naweza kurejea wakati gani uwanjani , lakini matibabu ambayo nayafanya sasa ni ya hali ya juu na natakiwa kupumzika muda mwingi ndio maana nimerudi nyumbani,"amesema.
Mshambuliaji huyo alimaliza nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora msimu uliopita 2020/21, akitanguliwa na mshambuliaji mwenzake wa Simba SC John Bocco.
Tags
Michezo