'Elimu ya usalama barabarani ikolezwe kwa waendesha bodaboda'

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha Usalama Barabarani kimeombwa kuendelea kutoa elimu inayolenga kuwapatia ufahamu zaidi waendesha bodaboda ili kuepuka ajali zinazosababishwa na ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Chuo cha Udereva WERENI kilichopo mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, Reuben Mushi wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Mushi alikuwa akiangazia kuelekea maadhimisho ya Siku ya Usalama Barabarani yanayotarajiwa kufanyika Novemba 16, mwaka huu jijini Arusha.
Amesema pamoja na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabani kuendelea kutoa elimu, bado elimu zaidi inahitajika hususani kwa vijana waendesha bodaboda, kwani ajili zinazotokana na pikipiki maarufu kama bodaboda ni nyingi zaidi kuliko zile zinazotokana na vyombo vingine vya moto.

"Moja ya sababu za ajali ni tabia ya baadhi ya madereva wa pikipiki kutokufuata matumizi sahihi ya barabara na sheria zinazoongoza usalama barabarani kuwa moja ya sababu hatarishi za ajali hizo,"amesema Mushi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani , Wilbroad Mutafungwa amekaririwa akisema kuwa mkakati mkubwa wa kwanza kwa jeshi hilo ni zoezi la kuendelea kutoa elimu kupitia madawati ya elimu.

Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya waathirika wa ajali za barabarani ni watembea kwa miguu nchini, huku asilimia 60 ikibakia kwa watumiaji wengine wa barabara kama vile waendesha bodaboda, baiskeli na magari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news