Gari aina ya Nissan Magnite yaingia rasmi katika soko la Tanzania

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Wawekezaji nchini wameshauriwa kuhakikisha wanazalisha na kuwekeza bidhaa zenye ubora halisi utakaowawezesha Watanzania kununua na kutumia bidhaa hizo ziaidi ya mara moja badala ya kununua mara kwa mara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nissan Tanzania, Christophe Henning ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa gari mpya aina ya Nissan Magnite.

Henning amesema, uwepo wa mazingira mazuri nchini Tanzania unawapa nafasi ya kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.

Amesema, kutokana na fursa hiyo wanaona ni vema kutangaza gari mpya ambayo inayofanya kununuliwa na watu wa kipato chochote cha chini,kati na juu ambalo lina ubora uliokidhi viwango.

Mkurugenzi huyo amesema, ni wakati wa watanzania kuchangamkia fursa ya gari hiyo kwani ni miongoni mwa magari ambayo yanalotumia mafuta kidogo katika safari zake.

Naye Meneja Masoko wa kampuni hiyo,Alfred Minja amesema, hali ya biashara nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili iliyumba kutokana na ugonjwa wa virusi vya Korona (UVIKO-19), lakini kwa sasa biashara zinaanza kurudi kama kawaida.

“Mazingira ya uwekezaji katika Serikali ya Awamu ya Sita yanaonekana kuwa na viashiria vya kuelekea pazuri, kwani serikali imeboresha miundombinu yake hususani katika ukusanyaji wa kodi na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji,”amesema Minja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news