HALMASHAURI ZAPEWA SIKU 30 KUKAMILISHA UJENZI WA MADARASA

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu ameziagiza Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa Madarasa ifikapo Desemba 15,2021.
Akikagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Mhe. Ummy amesema hakutakuwa na uchaguzi wa awamu pili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza hivyo ameziagiza Halmashauri zote kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa madarasa kwa wakati ili wanafunzi wote wanaofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wanaanza kusoma kwa wakati mmoja.

Amesema, fedha za UVIKO 19 zimetolewa kwa lengo la kuendeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya, na elimu hivyo Viongozi wa Mikoa yote nchini wanawajibu wa kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ukamilishaji wa ujenzi wa miradi kwa wakati.

Waziri Ummy ametoa maelekezo juu ya kutumia mapaa yenye migongo miwili ili kupunguza gharama za ujenzi na kuhusu matumizi ya vigae amewataka kutumia tarazo au sakafu za kawaida kwa kuwa vigae vinavyowekwa kwenye ujenzi wa madarasa vipo chini ya viwango.

Aidha, kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai imepata kiasi cha shilingi milioni 860 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 42

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news