NA MWANDISHI DIRAMAKINI
UNGANA na Mkurugenzi wa Kitengo cha Udhibiti wa Mionzi wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ( (TAEC),Dkt. Justine Ngaile aweze kukupa maarifa zaidi juu ya utaratibu huo.
FAHAMU
Mbali na hayo, mara kwa mara Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imekuwa ikiendesha mafunzo juu ya usimamizi wa usalama wa mionzi kwa wafanyakazi wanaotumia vifaa vitumiavyo mionzi migodini, viwandani na kwa watengenezaji wa vifaa vya mionzi vya hospitalini.
Lengo kuu la mafunzo ni kutoa elimu kuhusiana na mionzi, matumizi salama ya mionzi, madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mionzi, Sheria inayosimamia udhibiti wa matumizi salama ya mionzi, namna bora ya kujikinga dhidi ya madhara ya mionzi kwa kuzingatia kanuni za ulinzi wa mionzi (Radiation Protection Principals) katika kuhakikisha usalama wa watumiaji na watengenezaji wa mashine za Midaki (X-Ray Baggage Scanner).