IGP Sirro apangua makamanda wa polisi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefanya uhamisho na mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 10, 2021 na msemaji wa jeshi la polisi, David Misime imeeleza kuwa, waliohamishwa ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Juma Bwire ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai.
Amesema nafasi ya Bwire inachukuliwa na aliyekuwa Afisa Mnadhimu mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Allan Bukumbi.

Amemtaja mwingine ni aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Kanda Maalum Dar es Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi, Ali Makame Hamad ambaye amehamishiwa Mkoa wa Katavi kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa huo kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga ambaye amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi, Marisone Mwakyoma amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma kuwa Msimamizi wa Ulinzi wa Miundombinu muhimu ya Serikali na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Zuberi Mwombeji sasa anakuwa Mkuu wa Operesheni Kanda Maalum Dar es Salaam.

Misime amesema uhamisho na mabadiliko hayo ni ya kawaida yenye lengo la kuboresha ufanisi katika kutekeleza jukumu la kulinda maisha ya watu na mali zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news