KATIKA JAMVILAHABARI LEO: TAHARUKI MBUNGE AUGUA UCHIZI

NA MWANDISHI WETU

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, ameombwa kuingilia kati na kumtaka baba mzazi wa Mbunge wa Jimbo la Mbogwe (CCM) amuachie mtoto wake ambaye ni mbunge wa jimbo hilo lililopo mkoani Geita, bwana Nicodamus Maganga ili apelekwe hospitali na kupatiwa matibabu ya ugonjwa wa akili unaomkabili kwa kipindi cha sasa.

Akizungumza bila kutaka kuandikwa gazetini, mmoja wa ndugu wa karibu wa mbunge huyo ameonyesha kumshangaa mzazi wao huyo kuona ni kwanini anamzuia ndugu yao asipelekwe hospitali hata kama wanahisi amepatwa na magonjwa ya kishirikina, lakini kwanza ilifaa ndugu yao awahishwe Mirembe.

‘’Uchizi ulimuanzia upya akiwa Sekenke, alipofika hapo alianza kumueleza dereva wake mambo ya ajabu huku akitaka amshushe kwenye gari, dereva alipambana sana hadi kumfikisha hapa nyumbani, tunashukuru amefika na tulipompokea tu wote tuliangua machozi,"alisema ndugu yake huyo.

"Kwa kweli tumeshawasiliana na ofisi ya Bunge na kwa uharaka mkubwa Bunge limetuma gari ya kubebea wagonjwa mahututi ili ndugu yetu apelewe Mireme Dodoma, tunashangaa kwa nini mzee anasema akae kwanza hadi siku tano zipite akipatiwa matibabu asili. Sijui lengo la mzee kwa.... Endelea kusoma gazeti la Jamvi la Habari Leo Novemba 17,2021.



2.MALALAMIKO BENKI KUPORA HEKALU MIKONONI MWA GAVANA

- Anayelalamika adai kuporwa kwa kughushiwa nyaraka, kuporwa na hatimaye kuuzwa kwa mnada bila kufuata utaratibu azidi kuchachamaa

- Aamua kumvaa Gavana wa benki kumueleza kinagaubaga ili aamue hatma ya haki yake..........

Kwa undani zaidi wa Habari hizi, usisite kutafuta nakala ya JAMVILAHABARI, ama JamviOnline TV ama Instagram, Facebook na Twitter.

👇👇👆👆👇👆👇👆


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news