NA MWANDISHI DIRAMAKINI
KMC FC kesho itashuka katika dimba la Uhuru lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Azam FC utakaopigwa saa 16:00 kamili jioni.
Mchezo huo wa mzunguko wa sita tangu kuanza kwa ligi kuu ya NBC , Timu ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Kocha mkuu John Simkoko itakuwa mwenyeji.
Kocha msaidizi wa KMC FC , Habibu Kondo amesema kuwa licha ya kuwa timu haina matokeo mazuri, lakini maandalizi yaliyofanyika katika kipindi hiki cha mapumziko yaliyokuwa yamepisha Timu ya Taifa yamefanikiwa kwa asilimia kubwa ikiwemo kurekebisha changamoto mbalimbali ambazo zilionekana katika michezo hiyo.
Habibu amefafanua kuwa hali ya kikosi ni nzuri ,ikiwemo morali za wachezaji ipo juu pamoja na fitness nzuri na kwamba licha kuwa mchezo wa kesho utakuwa na ushindani mkubwa lakini kwa maandalizi ambayo yamefanyika yataleta matokeo mazuri.
Kondo ameongeza kuwa, mipango ya Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni nikufanya vizuri katika michezo ya Ligi kuu ya NBC na kwamba licha ya kuwa na mwanzo ambao siorafiki lakini bado matumani makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho nimkubwa.
"Tunajua kuwa hatujaanza vizuri kwenye michezo yetu, lakini bado tupo kwenye ubora wetu, tumefanya maandalizi ambayo kimsingi yataleta matokeo chanya kikubwa mashabiki zetu wazidi kutupa ushirikiano.
"Tunaenda kucheza na Azam ambayo ni Timu nzuri na tunawaheshimu lakini tutapambana kuhakikisha kwamba tunaondoka na alama tatu kwani mchezo upo ndani ya uwezo,"amesema.
Tags
Michezo