NA MWANDISHI DIRAMAKINI
KIKOSI cha KMC FC leo kimefanya maandalizi yake ya mwisho kuelekea katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara hapo kesho dhidi ya Mbeya City utakaopigwa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya saa 16:00 jioni.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Novemba 26, 2021 na Christina Mwagala ambaye ni Afisa Habari wa KMC FC.
Mchezo huo wa mzunguko wa saba, KMC FC itakuwa ugenini, na kwamba hadi sasa benchi la ufundi kwa kushirikiana na wachezaji pamoja na viongozi limefanya maandalizi ya kutosha na kwamba kikosi kipo tayari katika mtangane huo.
Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya kocha Mkuu John Simkoko imejipanga vema kuhakikisha kwamba licha ya kuwa mchezo huo utakuwa na ushindani mkubwa, lakini kama timu kikubwa nikupambania alama tatu muhimu ambapo kimsingi mchezo huo bado upo ndani ya uwezowetu.
“Tunaifahamu Mbeya City kuwa ni timu nzuri, na tunacheza ugenini, lakini bado tupoimara na tunaingia uwanjani kutafuta alama tatu muhimu ambazo kimsingi kila mmoja anazihitaji na sisi KMC FC tumekuja hapa Mbeya kuzitafuta hizo pointi hivyo maandalizi ambayo tumeyafanya tangutulipokuwa Dar es Salaam hadi sasa yatakwenda kutupa matokeo chanya,"amesema.
Aidha, Timu ya KMC FC ilifika Jijini hapa jana salama, licha ya kwamba hali ya hewa ni baridi iliyotawaliwa na mvua na leo wachezaji wameamka salama natumefanya mazoezi vizuri katika uwanja ambao tutakwenda kuutumia hapo kesho kwenye mchezo wetu hivyo kikubwa tunamuomba mwenyezi Mungu atuamshe salama ili tukapambane uwanjani vizuri.