NA MWANDISHI DIRAMAKINI
UONGOZI wa Klabu ya Manchester United wamefikia makubaliano ya mdomo na kuachana na kocha wake Ole Gunner Solskjaer.
Hatua hiyo inafuatia matokeo mabaya mfululizo ikiwemo kipigo cha 4-1 kutoka kwa Watford Jumamosi ya Novemba 20, 2021 katika dimba la Vqcarage Road.
Huu ukiwa ni mwendelezo wa vipigo vya karibu.
Manchester United ilijikuta ikianza kupotea mapema ngwe ya kwanza kutokana na kushindwa kuhimili kishindo cha Watford katika mpira wa kasi na nguvu ambapo Scott McTominay alilazimika kumfanya madhambi Joshua King ndani ya eneo la hatari.
Ubora wa mlinda mlango wa Manchester United David de Gea uliisaidia timu hiyo kuwa salama baada ya kuokoa mara mbili penati ya Ismaila Sarr.
Magoli ya Watford ambayo kabla ya mchezo wa huo walikuwa hawajawai kushinda nyumbani yaliwekwa knyuvuni na Joshua King, Joao Pedro, Emmanuel Dennis na Ismaila Sarr.
Wakati bao pekee la Manchester United likifungwa na kiungo mshambuliaji Donny van de Beek akimalizia mpira wa staa wa klabu hiyo Cristiano Ronaldo.
Kipigo hicho kilifanya Manchester United kwa sasa kubakia nafasi ya saba na alama 17 wakati Watford wakiwa nyuma ya United kwa tofauti ya alama nne katika nafasi ya 16.
Aidha, baaada ya hapo, kikao cha saa 5 kilifanyika na hatimaye pande zote zimekubaliana kuvunja mkataba huo na makubaliano hayo kwa maandishi yatasainiwa baadae.
Hata hivyo, klabu kwa sasa itakuwa chini ya viungo wa zamani wa klabu hiyo Michael Carrick na Fletcher.