Liverpool yaiacha hoi Arsenal, yatembezewa 4-0 EPL

NA GODFREY NNKO

KLABU ya Liverpool imejizolea alama tatu zilizosindikizwa na mabao 4-0 dhidi ya Arsenal.Raha ya ushindi. (Picha na Getty Images).

Matokeo haya ya Novemba 20,2021 yanawafanya kuhitimisha ushindi wa mechi 10 mfululizo kwao baada ya kuvuna alama tatu wakiwa nyumbani katika dimba la Anfield. Ni katika mwendelezo wa mitanange ya Ligi Kuu nchini England – Premier League (EPL).
Magoli ya Liverpool inayonolewa na kocha Jurgen Klopp yamefungwa na Sadio Mane, Mohamed Salah, Diogo Jota na Takumi Minamino huku nyota wa mchezo huo akiwa ni Trent Alexander Arnold beki wa kulia baada ya kutoa msaada wa goli mbili kwenye ushindi huo.

Aliyeanza kuharibu mipango ya Arsenl ni Mane ndani ya dakika ya 39 ya kipindi cha kwanza, dakika ya 52 Jota aliweka bao lingine, Salah akaja kuongeza lingine dakika ya 73 ambapo Takumi aliongeza kilio Arsenal kwa kuachia bao la nne ndani ya dakika 77, hadi mwisho wa mtanange, ubao ulisoma Arsenal 0 huku Liverpool ukisoma mabao manne.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kukwea mpaka nafasi ya pili nyuma ya vinara Chelsea wakati Arsenal wakibakia nafasi ya tano.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema, licha ya kichapo hicho ambacho kinaweza kuleta ghadhabu miongoni mwa mashabiki wao, hawapaswi kuumia badala yake wajipe muda wakafanyie kazi kasoro walizobaini ili mchezo ujao waweze kufanya vizuri.

Pia amesema, wachezaji wake wanapaswa kutumia matokeo hayo ya kukatisha tamaa, kwa ajili ya kwenda kujiweka sawa ili kipindi kijacho waweze kutibu majeraha.

"Sipendi kujifunza hivyo, lakini kuna mafunzo mengi ambayo tunaweza kuchukua kutokana na mapungufu yetu katika mchezo huu.Jambo kubwa ni kutambua kuwa, kesho ijayo kwetu inapaswa iwe bora.

"Tutaangalia kile tulichopaswa kufanya vizuri zaidi na kwa nini tuliadhibiwa jinsi tulivyoadhibiwa na baada ya hapo kuweka nguvu zetu na kuzingatia mchezo unaofuata. Tutakwenda pia kuifanyia kazi safu ya ulinzi,"amesema Arteta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news