Mguu wa Albino uliokatwa, watoto 117 wa 'Ibilisi' wanaswa Tanga

NA HADIJA BAGASHA

Jeshi la polisi Mkoa wa Tanga limefanikiwa kuupata mguu wa mtu mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) uliokatwa hivi karibuni na watu waliokwenda kufukua kaburi lake wilayani Lushoto Mkoani Tanga kwa madai kuwa ukiwa na kiungo cha watu wenye ulemavu wa ngozi utajiri unakufuata.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Kamishna Msaidizi wa Polisi Safia Jongo amesema watu watatu wamekamatwa wakiwa na kiungo hicho ambapo tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Tanda mwezi Oktoba, mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli mkoani Tanga.

Awali akizungumza na waandishi wa habari Kamanda Jongo amesema tarehe Oktoba 26,2021 walipokea taarifa ya kufukuliwa kwa kaburi na kiungo cha mwili Heri Shehe Kijangwa (45) aliyezikwa Julai 4,2020 baada ya familia kuona kaburi limetitia na kutia shaka.Zinazohusiana soma, 'Tunakemea unajisi na wizi wa mabaki ya Heri Kijangwa'

Kamanda Jongo amesema, baada kupata taarifa Jeshi la Polisi lilienda kufukua kaburi ili kujua mwili upo au kuna nini kimefanyika na ndipo walipobaini kuwa mwili wa mtu huyo umefukuliwa na kukatwa mguu wa kulia.

Kamanda Jongo amesema baada ya tukio, polisi ilifanya msako na kufanikiwa kuwakamata watu watatu ambao walionyesha mguu huo walioukata na kuufukia kwenye shamba la mmoja wa watuhumiwa hao.

"Jeshi la Polisi liligundua kuwa kaburi lilifukuliwa na mwili wa marehemu upo isipokua mguu wa kulia umekatwa mguu huo uliofukuliwa na kukatwa katika kaburi wilayani Lushoto umepatikana na watu watatu wanashikiliwa kwa tukio hilo baada ya ushirikiano wa Jeshi la Polisi na uongozi wa wilaya, "amesema Kamanda Jongo.

Kamanda Jongo ameongeza kuwa baada ya tukio hilo Jeshi la Polisi lilianza msako na kuwakamata watu watatu waliohusika ambapo katika, mahojiano ya kwanini walifanya kitendo hicho walidai kuwa ukiwa na kiungo cha mlemavu wa ngozi basi utajiri unakufuata.Related posts,'We deplore the desecration and theft of the remains of Heri Kijangwa'

Kamanda Jongo amesema Novemba Mosi, 2021 majira ya saa kumi jioni jeshi hilo liliwakamata watu watatu waliokiri kufukua kaburi kwa kushawishiwa na mtu ambaye bado anatafutwa,lakini wakakiri kiungo hicho kipo na wamekifukia na jeshi la polisi limekiri kukipata.

Hata hivyo, watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa ajili ya taratibu za kisheria wamekiri kuwa ni maneno ya vijiweni ndio yaliyowashawishi kwa kuambiwa ukiwa na kiungo cha Albino utajiri utakufuata.

Kamanda ametoa wito na kuwatoa taharuki watu wenye ulemavu wa ngozi,(Albino) na jamii ya Tanga kuwa Mkoa wa Tanga ni salama na hauna tabia hiyo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Kamanda huyo amesema, uchunguzi unaendelea na watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio hilo kukamilika.

Katika tukio lingine kamanda Jongo alikiri kuwakamata watoto wa ibilisi 117 wenye umri kati ya 12 na 18 wanaounda vikundi vinavyoendesha matukio ya uporaji wa mali na kuwajeruhi watu kwa mapanga, bisibisi na nyundo.Zinazohusiana soma,Wahitimu shule za msingi na sekondari watadharishwa kuhusu 'watoto wa ibilisi'

Kamanda Jongo amesema, baada ya watoto hao kukamatwa wamekabidhiwa kwa wazazi wao kulingana na umri wao kuwa mdogo huku wengine wamefikishwa mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.

Amesema wazazi wanne wa watoto hao walikamatwa kwa kosa la kushindwa kuwalea watoto wao na wao watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Katika kuzuia na kupambana na uhalifu jeshi hilo kwa kipindi cha mwezo Oktoba limefanikiwa kukamata jumla ya silaha 12 pamoja na moja ya bastola iliyokuwa ikimilikiwa na mtuhumiwa mmoja,na nyingine 11 ni magombore.Unaweza kusoma,Msako wa 'Watoto wa Ibilisi Tanga' waanza, IGP Sirro atoa maagizo ya haraka

Amesema na silaha hizo zilikuwa zinamilikiwa kinyume na sheria na watu sita wamekamatwa.

Wakati huo huo Kamanda Jongo amesema, wanawashikilia watu 65 ambao ni raia kutoka nchini Somalia, Ethiopia na Kenya walioingia nchini bila kibali,na watanzania wanne waliokuwa wakiwavusha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news