NA MWANDISHI MAALUM
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa David Silinde amezindua Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Tanzania na kuwaagiza viongozi hao wakasimamie fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao.
Naibu Waziri Silinde ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na viongozi na wajumbe wa umoja huo ambao moja kwa moja ndio walengwa katika maeneo wanayoishi na wananchi kwa kuona na kusimamia maendeleo ya miradi inayopelekwa ujenzi wa miundombinu huduma za kiuchumi na kijamii ikiwemo Elimu, Afya na Barabara.
Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inatambua mchango na jitihada za Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji nchini zikiwemo pamoja na changamoto amesema Naibu Waziri Silinde katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 Serikali imezitaka Halmashauri zote nchini kutoa fedha za ujenzi, kukarabati pamoja na ununuzi wa samani za ofisi hizo ili viongozi hao waweza kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akifafanua stahiki za viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Serikali imeweka utaratibu kwa kila Mtaa au Kijiji kulipa posho kutokana na mapato yao.
Halmashauri zote nchini hupaswa kurejesha mapato ya Kijiji/Mtaa yanajumuisha mapato yanayotokana na asilimia 20 ya mapato yanayokusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya Halmashuri nakiri kwamba utekelezaji wake unatofautiana kati ya Halmashauri moja na nyingine”. Amesema Silinde
Amewaagiza viongozi wa umoja huo kuisaidia Serikali katika kushirikiana na Watendaji wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu ili kuzipa heshima Mamlaka za Serikali za Mitaa lakini pia kutatua changamoto za wananchi hasa migogoro ya ardhi nchini kwani hili linaanzia kwao.
"Hakikisheni mnaepuka kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi katika maeneo yenu kwa kushiriki kuuza au kushuhudia uuzaji wa ardhi kwa mnunuzi zaidi ya mmoja na bila kuzingatia Sheria ikiwemo maeneo ya wazi, maeneo yaliyoifadhiwa au maeneo ya kingo za mito na bahari kinyume na Sheria,” amesema Silinde
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa Serikali 20za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Tanzania (UWETA) Bw. Lucas Mwasongwe ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango wao na kuiomba iendelee kuona umoja huo kwani wao wanafasi kubwa kwa jamii katika kuleta maendeleo ya nchi.
Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Tanzania utaunganisha Wenyeviti wa Mitaa 4,263, Vijiji 12,318 na Vitongoji 64,361 nchini.
Tags
Habari