Mwalimu Makuru afunguka mambo mazito kuhusu viongozi waliochaguliwa,wateule

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Mjini mkoani Mara, Mwalimu Makuru Lameck Joseph amesema umefika wakati kwa viongozi wa Serikali kushirikiana na viongozi waliochaguliwa na wananchi ili kutatua matatizo yanayoikabili jamii yetu kwa sasa.

Amesema kumekuwepo hulka na kasumba mbaya ya baadhi ya viongozi hususani wateule wa Rais kutokuwa na ushirikiano mzuri na wawakilishi wa kuchaguliwa hususani madiwani na wabunge, ambapo kuna baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yanamhusu mwananchi muda mwingi yamekuwa yakikosa suhuhisho kutokana tu na baadhi ya viongozi kutokuwa pamoja katika kutatua matatizo hayo ya wananchi.
"Kwa mfano, suala la wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu WAMACHINGA limekuwa ni tatizo kubwa katika jamii yetu kutokana na baadhi ya wabunge kushindwa kukaa na wananchi wao pamoja na watendaji wa serikali hususani Wakurugenzi na wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa kumekuwa na kero nyingi sana kwa wamachinga ambazo kimsingi nyingi zimeshindwa kutatuliwa.

"Hali hiyo inatokana na baadhi ya viongozi wa wananchi hususani madiwani na wenyeviti wa halmashauri, wabunge, wakuu wa wilaya na mikoa kushindwa kutatua kero zao kwa pamoja na kuwa na mashirikiano, baadhi ya tabia ya viongozi wa serikali wananchi hususani wadiwani na wabunge ndiyo chanzo cha kuwepo kwa malalamiko ya wananchi na kero nyingi zimeshindwa kutatuliwa kwa wakati, hivyo ni kutokana na viongozi waliteuliwa na Rais na waliochaguliwa na wananchi kushindwa kutambua kwamba wote wanafanya kazi kwa niaba ya wananchi na si vinginevyo.

"Hivyo lazima waweke mbele maslahi ya wananchi pasipokujali ITIKADI za vyama vyao na pasipo kujali mirengo yao ya kisiasa na kimitazamo, bali wajue mwananchi anachotaka ni maendeleo awe na maisha bora na aweze kupata kipato na wananchi wanachohitaji ni huduma bora za afya, maji,elimu, miundombinu bora pamoja na msalahi mazuri kwa watumishi na sio migogoro yao,"Mwalimu Makuru ameyabainisha hayo katika mahojiano maalum na DIRAMAKINI Blog.

Pia Mwalimu Makuru amesema kuwa, "naomba kuhimiza kumekuwa na migogoro ya wamachinga na serikali, ushauri wangu ni kweli kabisa usiopingika lazima tuweke njia vizuri na tupange maeneo maalum ya wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga), lakini lazima tujue tunapowapeleka lazima pawe na uhakika wa kufanya biashara, hivyo lazima viongozi wa wananchi hususani wabunge, madiwani na wakurugenzi wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya kwa pamoja na kuchagua maeneo maalumu kwa ajili ya biashara na maeneo hayo yawe rafiki kwa ajili ya biashara zao na sio kuwapeleka nje ya mji ama pembezoni,”amesema Mwalimu Makuru.

Kada huyo amesema, kuna njia zingine tunaweza kuwa tunafanya kwa kufunga mtaa angalau siku moja kwa wiki ili wananchi waweze kufanya biashara waweze kupata kipato, hivyo serikali kuna haja ya kuliangalia hilo kama itawezekana.

"Kumekuwa na changamoto kubwa kwa hivi sasa hususani katika miji yetu na majiji yetu hapa nchini kuhusu suala la wamachinga au wafanyabiashara wadogowadogo ambalo limekuwa gumzo sana katika jamii yetu, kwani serikali imefanya mpango wa kuwatengea wafanyabiashara maeneo maalumu ya kufanyia biashara zao hususani wamachinga hivyo kutokana na hali hiyo iliweza kuleta hali ya sintofahamu miongoni mwa wafanyabiashara hao maarufu wamachinga ambapo kuna baadhi ya maeneo waliokuwa wametegewa hawakutaka kwenda, hivyo kuleta hali ya sintofahamu ambapo kuna baadhi yao walifungiwa vitu vyao na kwa ushauri wangu mgogoro huu ulikuwa unatakiwa wadau wote kabla ya kuanza kuwaondosha wafanyabiashara hao maarufu wamachinga wakae kwa pamoja ili wakubaliane njia zipi bora za kutumia pasipo kumuumiza mtu yoyote yule ndipo hatua zingine zifuate.

"Pia kuna baadhi ya maeneo ya mjini ambapo kuna viwanja vya wazi na mchezo hususani kati kati ya mji ndipo yangetumika kwa kuwategea wafanyabiashara hao hayo maeneo mfano kuna viwanja vya mpira viko katikati ya mji,"amesisitiza Mwalimu Makuru.

"Rai yangu na ushauri kume kuwa na mazoea kwa wabunge wengi kutokurudi kwa wananchi majimboni na kufanya vikao na mikutano na wananchi wao ili kuwapa taarifa wananchi kwa kilichojadiliwa katika bunge na wananchi wawe wanajua ni kitu gani kinachoelea na serikali imepanga kumfanyia nini wananchi, hivyo nawaomba wabunge waweze kuwa wanakuja kuwapa wananchi mrejesho kwa walichojadili bungeni pia na kutembelea wananchi ili kujua kero zao zinazowakabili wananchi na kuzitatua. Hapa kuna haja ya wabunge kujua mabosi wao ni wananchi waliowachagua na si vinginevyo,"amefafanua Mwalimu Makuru.
 
Kada huyo amesema kuwa, wanapaswa kuweka mbele maslahi ya wananchi waliowachagua na kuwasemea.

"Pia kuna migogoro mingine imekuwa inatokana na ITIKADI au MIRENGO kuwa tofauti ambayo imekuwa ikifanya wananchi kuteseka kwa kutopata huduma bora ambayo ni stahiki zao na haki kupata hizo huduma ila sababu tu ya itikadi au MIRENGO kuwa tofauti wananchi wanapata kero na zinashindwa kutatuliwa kwa wakati.
 
"Migogoro mingine imetokana na FIKRA na MITAZAMO tofauti nayo imechangia katika jamii zetu kuumia sana, pia kwa mfano kwa baadhi ya wabunge walikuwa ni wakuu wa mikoa yaani wateule wa Rais hapo kipindi cha nyuma na hivi sasa wamechaguliwa na wananchi kuwa wabunge ila bado wana mitamo ya kifikra kwa kuzani kwamba bado ni wateule wa Rais, wakati hivi sasa ni viongozi wa kuchaguliwa na wananchi hivyo walipaswa kuwatetea wananchi na kuwawakilisha wananchi wanaletewa maendeleo na wananchi na kuwatetea ila wao wameendelea kuwa na migogoro maofisini baina yao wakurugenzi na wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ambapo mwisho wa siku migogoro hiyo wananchi ndio wanaoumia kwa kukosa maendeleo.

"Hususani kuna baadhi ya maeneo suala la wamachinga nguvu kubwa ilitumika sana kwa wananchi ambapo baadhi ya maeneo askari mgambo walitumia nguvu sana utazani wao nao ni serikali ndogo, kumbe sivyo. Hivyo basi lazima viongozi walichanguliwa na kuteuliwa wafanye kazi kwa pamoja na kwa maelewano na mshikamano ili iweze kuleta tija kwa maendeleo ya wananchi na kwa taifa kwa ujumla,"amesema Mwalimu Makuru.
 
Aidha, Mwalimu Makuru amehitimisha kwa kusema kuwa, "Kumbukeni nyie ni viongozi mliochaguliwa na mlioteuliwa, mtambue kuwa cheo ni dhamana na uongozi ni dhamana, hivyo tendeni wajibu wenu kwa maslahi ya Taifa. Mola ibariki Tanzania, ibariki Afrika,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news