Mwenyekiti wa Kitongoji amuua mkewe na yeye kujinyonga

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Augustini Moshi (37) ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Uruwa "B" na mkazi wa Kijiji cha Mfuruashe Kata ya Mengeni chini Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro anadaiwa kumuua mkewe na yeye mwenyewe kujiua kwa kujinyonga.

Kamishina Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, ACP Simon Maigwa ameyasema hayo mjini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

ACP Maigwa alimtaja Augustini Moshi ambaye anatuhumiwa kumuua mkewe Atanasia Moshi (31) mchaga na mfanyabiashara kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shin
goni na kisha yeye mwenyewe kujiua.

"Tukio hili lilitokea katika Kata ya Mengeni chini, tarafa ya Mengwe Wilaya ha Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambapo mtu mmoja aitwaye Atanasia Moshi (31) mchaga na mfanyabiashara, mkazi wa kijiji cha Mfuruashe aliuawa na mume wake aitwaye Augustini Moshi (37) ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji,"amesema ACP Maigwa.

Alidai kuwa, marehemu Atanasia Moshi na mume wake walikuwa kwenye mgogoro wa kimapenzi kwa hadi pale umauti ulipowakuta na miili yao kugundulika usiku wa kuamkia Novemba 8, mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi.

Kamanda Maigwa amesema Augustini Moshi mara ya kutekekeza mauaji hayo na yeye mwenyewe aliamua kujinyonga kwa kutumia waya alioufunga juu ya kenchi ya paa la nyumba yake.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa, chanzo cha tukio hilo ni mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia uliosababishwa na wivu wa kimapenzi, upelelezi zaidi unaendelea ambapo kwa sasa miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Huruma kwa ajili ya uchunguzi zaidi,"amesema.

ACP Maigwa ametoa wito kwa jamii kutambua changamoto zilizopo katika familia ili kuweza kutafuta njia madhubuti za kuzindoa pindi zinapojitokeza ili kuepusha hali kama hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news