NA MWANDISHI MAALUM
KIONGOZI Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania,Nabii Dkt. Joshua Aram Mwantyala amesema kuwa, kuanzia Jumamosi hii ya Novemba 13, 2021 ataanza kuachilia uponyaji wa papo kwa papo ukiwa sebuleni kwako na familia.
Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania ambayo huwa inawakutanisha maelfu ya watu kutoka ndani na nje ya nchi ina makao yake makuu Yespa Kihonda mjini Morogoro.
Nabii Dkt.Joshua ambaye pia ni Rais wa New Covenant Unity International (NCUI) ameyasema hayo leo Novemba 11, 2021 wakati akizungumzia kuhusiana na ujio wa mahubiri ya moja kwa moja kupitia runinga ya Star TV.
"Nina furaha sana kwa kuwa, Mungu aliyeniita kwa ajili ya kuhubiri habari njema ya neno lake na kuachilia uponyaji kwa jina la Yesu Kristo ameendelea kupanua wigo wa kufikisha ujumbe wa neno lake kwa njia mbalimbali.
"Tumekuwa tukirusha vipindi mbalimbali moja kwa moja kupitia redio na mitandao ya kijamii na hakika wengi wameepokea uponyaji na sasa wanaendelea kumtukuza Mungu kwa matendo makuu aliyoyafanyia kupitia Sauti ya Uponyaji. Sasa, Mungu amenipa maono ya kusonga mbele zaidi na sasa niseme wazi kuwa,tutaanza kurusha vipindi vyetu rasmi kuanzia Jumamosi hii katika runinga ya Star TV.
"Ni Jumamosi wiki hii kuanzia saa tatu na nusu usiku, hivyo usipange kukosa, hii ni ibada yenye nguvu kubwa, kwani kila mwenye hitaji lake wakiwemo wagonjwa, waliofungwa katika vifungo vya shetani na kila aina ya mateso Mungu wetu wa Mbinguni atakwenda kuwafanyia mambo makuu sana,"amesema Nabii Dkt.Joshua.
Tags
Habari