NA VERONICA MWAFISI
NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Watumishi wa Umma kutekeleza majukumu yao kikamilifu kwani kwa kutofanya hivyo ni dhambi kubwa ambayo imekatazwa katika vitabu vyote vya dini.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Bibi Pili Mnyema alipotembelea Ofisi ya Katibu Tawala huyo kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF jijini Tanga.
Akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Jijini Tanga, Mhe. Ndejembi amesema, kuna baadhi ya Watumishi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kutotekeleza majukumu yao kikamilifu jambo ambalo linapingana na vitabu vyote vya dini.
“Tunaweza kusema tuna watumishi laki tano na zaidi lakini tujiulize je ni wangapi wanaotimiza wajibu wao ipasavyo? Baadhi ya watumishi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kutengeneza mazingira ya rushwa, huu sio utumishi wa umma tunaoutaka, utumishi wa umma tunaotaka kuuona ni wa kila mtumishi kufanya kazi kwa weledi wa hali ya juu, bila ubaguzi wa aina yoyote na kutumia maarifa pasipo kushurutishwa,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.
Mhe. Ndejembi ameongeza kuwa, ni lazima Watumishi wa Umma wajitafakari kama wametimiza wajibu wao kikamilifu hasa pale wanapodai haki zao ikiwemo kupandishwa madaraja, mishahara na stahiki nyingine.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo kwa Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hiyo.
Akizungumzia uwajibikaji kwa taasisi za umma, Mhe. Ndejembi amesema kuwa kuna maeneo mengine taasisi za umma hazizungumzi katika utekelezaji wa majukumu yao, akitolea mfano wa taasisi inayohusika na ujenzi wa barabara kuwa baada ya kukamilika kujengwa ndipo taasisi nyingine mfano Tanesco au Mamlaka ya maji wanachimba kupitisha mabomba na kuongeza kuwa huku sio kutimiza wajibu.
“Kuna maeneo mengine unakuta zote ni taasisi za umma, lakini hazizungumzi, kwa mfano barabara ya lami inajengwa kwa gharama kubwa, kesho unakuta wengine wanakuja na sululu wanachimba ili kupitisha bomba chini, mlishindwa kuwasiliana na kupanga mipango mapema kujua kuwa hili litafanyika? Mhe. Ndejembi ameuliza na kuongeza kuwa kufanya hivyo ni kutotimiza wajibu, jambo ambalo sio utumishi wa umma tunaoutaka” Mhe. Ndejembi ameongeza.
Mhe. Ndejembi amesema Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona wananchi wakihudumiwa kikamilifu, hivyo katika kufikia lengo hilo, ni jukumu la kila mtumishi kutekeleza majukumu pasipo kushurutishwa.
Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hiyo.
Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Dkt. Frank Makunde, akiwasilisha hoja za kiutumishi kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hiyo.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akifafanua hoja zilizowasilishwa na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Bw. Isaya Mbenje akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mhe. Ghaibuazi Lingo mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
“Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kutoa huduma bora kwa wananchi, hivyo tumsaidie kutekeleza majukumu yetu kikamilifu kwa kusikiliza kero na kutofanya kazi kwa matukio yaani kusubiri jambo kutokea ndipo mtumishi aanze kuchukua hatua,” Mhe. Ndejembi ameongeza.
Akitoa neno la shukrani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Bw. Isaya Mbenje amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kufanya ziara katika halmashauri yao na kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao.
Bw. Mbenje amemuahidi Mhe. Ndejembi kuwa yeye pamoja na watumishi wenzake watayafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa ili kuleta maendeleo ya nchi.
Mhe. Ndejembi ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu ya kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma na kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Jiji la Tanga ambapo leo alikuwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.