NA MWANDISHI DIRAMAKINI
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametoa pongezi kwa Umoja wa Maaskari Wastaafu (UMAWA), kwa kujenga chombo hicho ambacho kinawaweka pamoja askari waastaafu.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Novemba 28, 2021 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Umoja wa Maaskari Wastaafu (UMAWA), Ikulu jijini Zanzibar wakati walipofika kwa ajili ya kujitambulisha na kumjulisha Rais nia na dhamira za umoja huo.
Rais Dkt. Mwinyi alitoa pongezi kwa mafanikio yaliyopatikana katika umoja huo kwa kuendeleza miradi kadhaa ikwiemo ulinzi, mradi wa ulazaji wa gari,milango ya maduka na mradi wa kituo cha mafuta huku akipongeza lengo la umoja huo la kuanzisha miradi mipya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya UMAWA, walipofika Ikulu kwa mazungumzo ukiongozwa na Mwenyekiti wake Bw.Mussa Miraji Vuai (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).
Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitoa kauli kwa uongozi huo kwamba kwa zile taasisi zote za Serikali zinazodaiwa na UMAWA atahakikisha zinalip a
madeni yake kama alivyoeleza azma hiyo hivi karibuni katika hotuba yake
ya mwaka mmoja tokea aingie madarakani kwa kupitia zile fedha za mkopo
za UVIKO-19 baada ya kuzingatia uhakiki.
Rais Dkt.
Mwinyi pia, alieleza haja kwa UMAWA kufuata taratibu na kanuni za ushirika kama ulivyosajiliwa pamoja na kufuata Katiba yake ili kuondosha
manunguniko kwa wanachama na hatimae kuiwezesha Serikali kuwauga mkono.
Pamoja na hayo, Rais Dk. Mwinyi alieleza azma ya
Serikali ya kutengeneza kituo kikuu cha Mabasi cha aina yake hapa
Zanzibar katika eneo la Kijangwani ambacho kitakuwa na maduka pamoja na
huduma nyengine ambapo anamatumaini kwamba Umoja huo utafaidika na mradi
huo iwapo wataridhia.
Rais Dkt. Mwinyi, alieleza kwamba kwa vile kundi hilo ni kubwa na kwa vile Serikali imeamua kuviwezesha vikundi mbali mbali basi kikundi hicho nacho kwa vile kina sifa zote za kusaidiwa basi hilo linawezsekana.
Nao
Umoja wa Maaskari Wastaafu (UMAWA), katika risala yao iliyosomwa na
Mwenyekiti wake Kanali Mstaafu Miraji Mussa Vuai, ulimpongeza Rais Dk.
Mwinyi kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi pamoja na kupongeza kwa kutimiza mwaka mmoja
madarani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya UMAWA Zanzibar, mazungumzo yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Mussa Miraji Vuai akiwa na ujumbe wake.(Picha na Ikulu).
Aidha,
uongozi huo ulimpongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kujenga na kusimamia
nidhamu, uwajibikaji na heshima kazini inayoleta utawala bora bila ya
muhali huku akisimamia haki za wananchi kwa nguvu zake zote.
Pia,
watoa pongeza kwa Rais Dkt. Mwinyi kwa kupambana na udhalilishaji na
ukatili wa kijinsia na watoto, kupiga vita dawa za kulevya, kuwajali na
kuwanyanyua wazee na vijana,kuimarisha huduma za kijamii na kuleta
maendeleo na wepesi wa maisha pamoja na kueleta maendeleo ya kiuchumi
kwa kuwawezesha wananchi kupunguza umasikini.
Uongozi
huo ulieleza kwamba wamekusudia kwenda na wakati kwa kujipanga kwenda
sambamba na Sera ya uchumi wa buluu inayohimiza ujenzi wa viwanda na
uvuvi wa bahari kuu.
Hivyo, uongozi huo waliomba
kupatiwa nyenzo za uvuvi kama vile boti, mishipi, nyavu na zana nyengine
ambazo zinaendana na hali ya uvuvi wa kisasa, kwani tayari wanao vijana
mahiri ambao wanawaandaa kwa kazi hiyo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Uongozi wa UMAWA Zanzibar baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu. Uongozi huo ulimpongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kuimarisha usalama, amani,
utulivu na utengamano nchini wka kuondoa chuki na uhasama wa kisiasa na
ukabila sambamba na kuvijenga vyombo vya ulinzi, usalama na sheria.
Mwenyekiti
huyo alieleza kuwa UMAWA inafuata mfumo wa kidemokrasia wa uongozi
unaoheshimu utawala wa sheria, haki za binaadamu, amani, usawa, haki,
heshima na uadilifu.
Uongozi huo ulieleza dhamira ya UMAWA ikiwa ni pamoja na kuimarisha hali ya Wastaafu kiuchumi na
kimaisha ili kupunguza ukali wa maisha pamoja na kuendeleza shughuli za
ulinzi wa Taifa na kuwafunza uzalendo vijana wa Zanzibar.
Sambamba
na hayo, umoja huo ulieleza changamoto inazozikabili ikiwa ni pamoja na
baadhi ya Taasisi kulimbikiza madeni kwa huduma za ulinzi na usafi
wanazotoa na kukwamisha shughuli zao.