NA MWANDISHI MAALUM
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefungua Kongamano la Tatu la Arusha kuhusu Ubora wa Taasisi za Umma katika Bara la Afrika na kueleza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatekeleza maazimio yatakayopitishwa na kongamano hilo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Mhe.Omar Said Shaaban pamoja na Mwenyekiti wa Pan African Center for Policy Studies Bibi Judica Amri-Lamson (kulia) wakati alipowasili Hoteli ya Verde Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi leo katika Ufunguzi wa Kongamano la tatu la Arusha kuhusu Ubora wa Taasisi za Umma “The Third Edition of The Arusha Symposium on the Quality of Public Institition”. (Picha na Ikulu).
Rais Dk. Mwinyi ametoa kauli hiyo leo wakati alipokuwa akifungua Kongamano la Tatu la Arusha kuhusu Ubora wa Taasisi za Umma lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde, Zanzibar na kutoa shukurani kwa uongozi wa Taasisi ya ‘Pan African Center for Policy Studies’ kwa kuchagua kufanya Kongamano hilo hapa Zanzibar.
Katika maelezo yake Rais Dkt. Mwinyi alisema kuwa, malengo na historia ya kuanzishwa eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA), ndio kunaweza kukusaidia kufahamu vyema umuhimu wa ushiriki wa watu wa jinsi zote bila ya ubaguzi.
Alisema kuwa, katika karne hii ya 21 nafasi ya mwanamke katika sekta ya biashara na ujasiriamali imezidi kunanuka.
Aliongeza kuwa idadi ya wanawake wanaojishughulisha na biashara katika ngazi ya Taifa katika nchi mbali mbali barani Afrika imeongezeka na vile vile idadi ya wafanyabiashara wanawake katika ngazi ya Kitaifa duniani kote imeongezeka.
Alisisitiza kwamba maendeleo hayo ni lazima yaambatane na jitihada ya kutatua changamoto zilizopo ambazo ni kikwazo kwa wanawake katika maendeleo ya biashara.
Rais Dk. Mwinyi alieleza kwamba licha ya mafanikio yaliyopatikana barani Afrika baada ya kuundwa kwa Umoja wa Afrika, kulionekana kuna haja ya kuwa na eneo Huru la Biashara Barani Afrika, ili kuimarisha maendeleo ya kiuchumi pamoja na kuimarisha uhusiano wa karibu baina ya raia wa nchi mbali mbali kupitia biashara. Baadhi ya washiriki wa Kongamano la tatu la Arusha kuhusu Ubora wa Taasisi za Umma “The Third Edition of The Arusha Symposium on the Quality of Public Institition”wakiwa katika Hoteli ya Verde Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo leo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alifungua Kongamano hilo.(Picha na Ikulu). Mwenyekiti wa Pan African Center for Policy Studies Bibi Judica Amri-Lamson (kulia) wakati alipokuwa akitoa maelezo yake katika Kongamano la tatu la Arusha kuhusu Ubora wa Taasisi za Umma “The Third Edition of The Arusha Symposium on the Quality of Public Institition” lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) katika Hoteli ya Verde Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi leo. (Picha na Ikulu).
Alisema kuwa Umoja wa Afrika uligundua kuwa kuna mapungufu makubwa katika ushirikiano wa kiuchumi na biashara hata kwa zile bidhaa na huduma ambazo zinaweza kupatikana miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja huo.
Aliongeza kuwa faida kubwa ya umoja huo ni kuendeleza uchumi kwa kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji miongoni mwa nchi za Afrika hatua ambayo utekelezaji wake utawezesha nchi wanachama wa Umoja wa Afrika hatimae kufikia umoja wa Forodha.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe.Omar Said Shaaban alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) kulifungua Kongamano la tatu la Arusha kuhusu Ubora wa Taasisi za Umma “The Third Edition of The Arusha Symposium on the Quality of Public Institition” leo katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi. Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe.Martin Ngoga (kulia) akitoa akitoa salam zake katika Ufunguzi wa Kongamano la tatu la Arusha kuhusu Ubora wa Taasisi za Umma “The Third Edition of The Arusha Symposium on the Quality of Public Institition” ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kushoto) amelifungua Kongamano hilo katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi.[Picha na Ikulu] 08/11/2021. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa hutuba yake ya kulifungua Kongamano la tatu la Arusha kuhusu Ubora wa Taasisi za Umma “The Third Edition of The Arusha Symposium on the Quality of Public Institition” hafla iliyofanyika leo katika Hoteli ya Verde Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikati) Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe.Omar Said Shaaban (katikati) na Mwenyekiti wa Pan African Center for Policy Studies Bibi Judica Amri-Lamson (kulia) wakisimama wakati Wimbo wa Taifa Ukipigwa katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Mkoa wa Mjini Magharibi leo katika Ufunguzi wa Kongamano la tatu la Arusha kuhusu Ubora wa Taasisi za Umma “The Third Edition of The Arusha Symposium on the Quality of Public Institition”. (Picha na Ikulu).
Aidha, Rais Dk. Mwinyi alipongeza Kauli mbiu ya Kongamano hilo isemayo “Nafasi ya Wanawake Barani Afrika katika kukabiliana na Changamoto za kimfumo zilizopo ili utekelezaji wa Malengo ya Kuanzishwa kwa Eneo Huru la Biashara Afrika yaweze kufikiwa”. Alieleza kwamba ni kauli mbiu nzuri kwani bila ya kushirikishwa wanawake kikamilifu katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya biashara na ujasiriamali hakutoweza kupatikana mafanikio, siyo tu katika utekelezaji malengo ya eneo Huru Barani Afrika, bali pia, katika utekelezaji wa malengo na mipango ya kuanzishwa Jumuiya mbali mbali za Kikanda.
Nae Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban alieleza umuhimu wa kufanyika kwa Kongamano hilo hapa Zanzibar sambamba na Azimio la Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara kwa nchi za Afrika uamuzi ambao ulikuwa ni sehemu ya utekelezaji wa Agenda 2063 ya Maazimio ya Umoja wa Afrika yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi,biashara na huduma miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, Martin Ngonga kwa upande wake alisema kuwa Bunge la Afrika Mashariki kupitia nchi zake sita liliweza kuweka mikakati maalum katika kuhakikisha wanawake wanapewa nafasi stahiki.
Nao viongozi wengine waliopata fursa ya kuzungumza katika Kongamano hilo walieleza azma yao ya kuja kulifanya Kongamano hilo hapa Zanzibar na kueleza mafanikio yaliyopatikana katika hatua za kuimarisha sekta ya biashara, kuwawezesha wajasiriamali sambamba na kuwapa kipaumbele wanawake huku wakieleza namna wanavyounga mkono Uchumi wa Buluu ambayo ndio Dira ya uchumi wa Serikali ya Awamu ya Nane anayoiongoza Rais Dk. Mwinyi.