Rais Samia ateua viongozi nane leo

NA GODFREY NNKO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi nane wakiwemo wenyeviti wa bodi watano.

Taarifa ya uteuzi wa viongozi hao imetolewa leo Novemba 13, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu imesema Rais Samia amemteua Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Dk Florence Turuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TIC).

Pia amemteua Profesa Sylvia Temu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA), na Profesa Ahmed Mohamed amekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki (EASTC).

Aidha, Rais amemteua Dkt. Mwamini Tulli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na Jacob Kibona kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Wataalam ya Ununuzi na Ugavi (PSFTB).

Wengine walioteuliwa ni Dk Irene Isaka kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Dk Tumaini Katunzi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo hicho.

“Pia Rais amemteua Geofrey Mbanyi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB). Mbanyi alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bodi ya Wataalam ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB),” imesema taarifa hiyo ambapo uteuzi huo umeanza Novemba 9, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news