NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Mkutano Mkuu wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (COP26) umefunguliwa rasmi Oktoba 31, 2021 mjini Glasgow nchini Scotland.
Picha kwa hisani ya Enviromental Defense Fund
Katika mkutano huo, wawakilishi wa nchi 200 duniani akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wanatarajiwa kutoa maamuzi muhimu ya pamoja kuhusu mpango wa 2030 wa kuzuia majanga ya tabia nchi.
Pia kutokana na ongezeko la joto duniani na shughuli za uuzaji wa mafuta, wanasayansi wanaonya kwamba hatua za haraka zinahitajika ili kuepuka janga la mabadiliko ya tabia ya nchi.
Katika ufunguzi wa kikao hicho, taarifa ya ripoti ya mabadiliko ya tabia nchi iliyotolewa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) itawasilishwa kwa washiriki.
Ripoti ya WMO ya wanasayansi wa hali ya hewa italinganisha viwango vya joto duniani mwaka huu na miaka iliyopita.
Huu ni mkutano wa wiki mbili ambazo zitatawaliwa na mazungumzo ya kina ya kidiplomasia, yakiangazia namna ya kukabiliana na changamoto ya pamoja ya ongezeko la joto duniani.
Matukio makuu yanayopewa kipaumbale ni athari za mabadiliko ya hali ya hewa, zikiwa ni pamoja na ongezeko la joto duniani, mafuriko na kuongezeka kwa mioto ya misituni.
Aidha, rekodi za Umoja wa Mataifa zimeonyesha kuwa, muongo uliopita ulikuwa wa joto jingi zaidi, hali ambayo inapelekea wataalam kuonya kuhusu umuhimu mkubwa wa mikakati mahsusi ya kukabiliana na mabadiliko hayo.
Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa ni moja ya mikutano mikubwa zaidi ya kimataifa, na ulicheleweshwa kwa mwaka mmoja kwa sababu ya janga hilo.
Oktoba 31, 2021 katika hafla ya ufunguzi wa mkutano ho, maafisa wa Umoja wa Mataifa walianza kwa kuelezea masuala muhimu ya kujadiliwa kabla ya duru itakayowakutanisha viongozi wa juu kutoka nchi mbalimbali za dunia.
Mwenyekiti anayeondoka Carolina Schmidt aliyafungua mazungumzo ya Glasgow, kwa kuwataka waliohudhuria kukaa kimya kwa dakika moja, kwa heshima ya waliopoteza maisha kutokana na janga la Covid-19, tangu kufanyika kwa mkutano wa mwisho wa hali ya hewa, mnamo mwaka wa 2019.
Viongozi wa nchi mbalimbali wanatarajiwa kukusanyika leo Novemba Mosi, 2021 mjini Glasgow, kuhudhuria mkutano huo, ambao umetanguliwa na ule wa viongozi wan chi zenye uchumi mkubwa zaidi duniani maarufu kama G20 uliofanyika mjini Roma, Italia.
Wakati huo huo, rekodi zimeonyesha kuwa, muongo uliopita ulikuwa wa joto zaidi jambo lililohitaji zaidi hatua za haraka na pamoja.
Mkutano wa Umoja wa Mataifa ni moja ya mikutano mikubwa zaidi ambayo Uingereza imewahi kuandaa na ilicheleweshwa kwa mwaka mmoja kwa sababu ya janga hilo. COP inasimamia mkutano wa nchi wanachama na ni mkutano wa 26.
Mkuu wa Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani (WMO) hivi karibuni na mashirika mengine tisa ya kimataifa wametoa wito wa pamoja na wa dharura kwa serikali kuweka kipaumbele kwa hatua jumuishi za maji na mabadiliko ya tabianchi kutokana na athari zinazoenea za masuala hayo kwa maendeleo endelevu.
"Hatua za haraka zinahitajika kwa dharura kushughulikia matokeo yanayohusiana na maji na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanaathiri watu na sayari,"ilieleza barua iliyotolewa kwa pamoja na wakuu wa nchi na serikali ambayo ilitolewa kuelekea mkesha wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP26.