RAS Manyara:Kwa ukatili huu haikubaliki

NA MOHAMED HAMAD

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Manyara, Carolina Mthapula amesema, vitendo vya ukatili vinavyoendelea kujitokeza mkoani humo havikukubaliki kibinadamu, kiutu na hata kisheria.
Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Carolina Mthapula (wa pili kushoto) akizungumza na Eliza Anton (36) katika viunga vya hospitali ya Kiteto baada ya kukaa hapo kwa miezi miwili kufuatia kufanyiwa ukatili na mume wake. (PICHA NA MOHAMED HAMAD).

Mthapula ameyasema hayo akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto, alipoenda kumuona Bi. Eliza Antoni (36) ambaye alifanyiwa ukatili na mume wake kwa kuvunjwa mikono na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake.

"Haiwezekani mwanaume unaamua kumvunja mikono na kumjeruhi mke wako hivi hivi..huu ni ukatili wa hali ya juu sana, Serikali hatuwezi kuvumilia na kutfumbua macho hata kidogo,"amesema Katibu Tawala huyo.

"Huyu mama alipigwa sana..hebu naomba fungua mkono, alipigwa mpaka mikono hii ikawa imevunjika vunjika, huku nyuma alipigwa sana tu kwa fimbo, kila aliyemwona alikata tamaa kuwa huyu mama atapona na ataendelea kuishi.

"Leo nimefika hapa nimekuta yule mama aliyekuwa amelala kitandani, aliyekata tamaa ya maisha hajiwezi anazungumza kwa tabu, yuko nje na anatembea baaba ya kukaa hapa hospitali kwa zaidi ya miezi miwili na vile vidonda vimeanza kupona mkono umeanza kuunga. Jambo la kushukuru sana,"amesema.

Amesema, huu ni mfano hai ambao akina mama wanapatia mateso, wanapigwa wananyanyaswa, wengine wanapoteza maisha lakini huyu kwa kudra ya Mwenyezi Mungu amepina sasa ila amepata ulemavu wa maisha.

"Nitoe wito kwa wanaume wote hapa Manyara na hata wanawake wanao wapiga wanaume zao kama wapo waache mara moja, hili halikubaliki. Mkoa wa Manyara ni wa pili nchini kwa ukatili tumejipanga kupunguza ukatili huu ambao kwa sasa umeanza kuleta madhara kwa wananchi,"amesema.

Kwa upande wake mhanga huyo, Eliza Antoni (36) na majeruhi amesema kuwa ni vyema kabla mtu hajafanya maamuzi ya kupiga mke wake akae atafakari na amuombe Mungu kwanza kwani maamuzi mengine yana madhara makubwa.

Amesema siku hiyo akipigwa alijua hatopona kutokana na aina ya kipigo alichopata na kuokolewa na wasamaria waliokuwa wanapita njiani kwani hapakuwa na wa kumtetea baada ya mume wake kuamua kufanya ukatili huo.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Dkt. Pascal Mbota akizungumza mbele ya Katibu Tawala amesema walimpokea Eliza akiwa hoi hajitambui kutokana na majeraha aliyopata, lakini waliweza kuokoa maisha yake na sasa anaweza kuruhusiwa

Akizungumza na DIRAMAKINI BLOGA, Abasi Famau ambaye ni msaidizi wa kisheria Kiteto amesema ili Mkoa wa Manyara utoke kwenye nafasi ya pili kwa ukatili Kitaifa kunahitajika jitihada za wadau mbalimbali zikiwemo asasi za Kiraia ambazo zitaelimisha umma kuacha ukatili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news