Serikali yatoa Ndege kwa Stars kuwafuata Madagascar

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Katika kuelekea mchezo wa mkondo wa pili baina ya Tanzania na Madagascar utakaopigwa Novemba 14, 2021 wa kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022, Serikali ya Jamhuri wa Muungano Tanzania imetoa ndege ya AirBus’kwa ajili ya mchezo huo.  

Taifa Stars itakuwa na kibarua dhidi ya Madagascar mchezo utakaopigwa Novemba 14 baada ya kumalizana na DR Congo Novemba 11, 2021.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abas amesema, Serikali itatoa ndege kwa ajili ya mchezo huo ikiwa ni kuhakikisha timu inafanya vizuri nje ya uwanja na ndani ya uwanja.

“Labda tu niwaambie Serikali katika kuhakikisha tunasapoti michezo tutatoa ndege ya kwenda na kurudi kwa ajili ya mchezo huo, ndege hiyo itabeba wachezaji na benchi lote la ufundi, viongozi, wadau wa soka na waandishi wa habari kwa lengo la kwenda kuhabarisha watanzania,”amesema.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao amesema tayari wameshaanza maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Madagascar. 

“Tayari tumeshaanza maandalizi ya mchezo wetu ujao dhidi ya Madagascar, lengo ni kuhakikisha tunapata ushindi,”ameema Kidao huku Taifa Stars inaongoza Kundi J ikiwa na alama 7 sawa na Benin huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na DR Congo wenye alama tano.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news