TANESCO:Mikoa 11 itakosa umeme kwa saa 12

NA GODFREY NNKO

Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limetoa taarifa kuwa mikoa 11 ya Tanzania itakosa umeme kwa saa 12, siku ya Novemba 15, mwaka huu kutokana na matengenezo yanayofanywa na shirika hilo katika njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Iringa.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao makuu ambayo imefafanua kuwa, ueme utakatika kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 12 jioni ili kupisha matengenezo yanayolenga kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika Gridi ya Taifa.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo, kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Hata hivyo, TANESCO imewaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza. "Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika, toa taarifa dawati la dharura la wilaya kwa msaada zaidi au Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu:+255 222 194 400 na +255 768 985 100,"imefafanua taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news