NA MWANDISHI DIRAMAKINI
SEKTA zilizopo chini ya Wizara ya Uwekezaji kikiwemo Kituo cha Huduma za Uwekezaji Nchini (TIC) imedhamiria kupunguza vikwazo wanavyokumbana navyo wawekezaji nchini.

Lengo likiwa ni kuongeza mapato yatakayosaidia ujenzi wa miundombunu na kuboresha huduma kwa jamii ikiwa ni kuunga mkono dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha anawaondolea kero wananchi wake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Geoffrey Mwambe ameyasema hayo katika katika kikao kazi kilichowakutanisha wataalamu wa mifumo na wadau mbalimbali katika sekta ya uwekezaji.


Kikao chenye lengo la kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa wawekezaji hao, amesema mamlaka zote na taasisi zinazoshughulikia wawekezaji kuweka zinapaswa kuweka mfumo mzuri ili kupunguza msururu w upatikanaji wa leseni kwa wawekezaji hao.
Naye Mkurugenzi Mtandaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Dkt.Maduhu Kazi amesema, mfumo huo utaweza kurahisisha kutoa huduma bora kwa wawekezaji.