Tanzania yazidi kusaka mbinu za kuliongoza soko la utalii ndani na nje, Mheshimiwa Masanja akutana na wadau muhimu

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) leo amekutana na watendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda kwa lengo la kujifunza kuhusu uwekezaji katika Utalii wa Mikutano.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Bodi ya Mikutano ya Rwanda ,Kigali.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amekutana na watendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda kwa lengo la kujifunza uwekezaji kwenye Utalii wa Mikutano katika kikao kilichofanyika Kigali- Rwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na watendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda alipowatembelea kwa lengo la kujifunza uwekezaji kwenye Utalii wa Mikutano katika kikao kilichofanyika Kigali Rwanda.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utalii kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga (kulia) akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) na watendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda kuhusu uwekezaji kwenye utalii wa mikutano kilichofanyika katika ofisi za bodi hiyo Kigali nchini Rwanda.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Ariella Kageruka mara baada ya kikao cha kujadili uwekezaji kwenye Utalii wa Mikutano kilichofanyika katika ofisi za Bodi ya Maendeleo ya Rwanda Kigali nchini Rwanda.
Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Utalii,Wizara ya Maliasili na Utalii, Philip Chitaunga akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Utalii, Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Emmanuel Nsabimana mara baada ya kikao cha kujifunza uwekezaji kwenye Utalii wa Mikutano kilichofanyika katika ofisi za Bodi ya Maendeleo ya Rwanda Kigali nchini Rwanda.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) (katikati) katika picha ya pamoja na watendaji wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda mara baada ya kikao cha kujifunza uwekezaji kwenye Utalii wa Mikutano kilichofanyika katika ofisi za Bodi ya Maendeleo ya Rwanda Kigali nchini Rwanda.

Amesema kuwa Bodi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuvutia watalii wa mikutano kwa kushirikiana kwa karibu na Sekta Binafsi.

“Kwa mfano kuna ukumbi mkubwa wa mikutano unaomilikiwa na Serikali unaendeshwa na Sekta Binafsi na umefanikiwa kuvutia watalii wengi” ameongeza Mhe. Masanja.

Amesema kupitia ujuzi uliopatikana katika kikao hicho, Tanzania itaenda kuutumia ili kutangaza na kuvutia watalii wa mikutano kutoka ndani na nje ya nchi na hatimaye kuikuza Sekta ya Utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news