NA MWANDISHI MAALUM
MZEE Ramadhani Tonge ambaye aliwahi kuwa mkufunzi wa masuala ya picha katika vyuo vya uandishi wa habari jijini Dar es Salaam amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoifikia DIRAMAKINI Blog, Mzee Tonge amefariki dunia akiwa katika matibabu Hospitali ya Amana, Ilala mkoani Dar es Salaam na atasafirishwa kwenda Morogoro kwa maziko.
Kwa nyakati tofauti, Mzee Tonge alitoa huduma ya ukufunzi katika Chuo cha Uandishi wa Habari cha Times Shool of Journalism (TSJ) cha Ilala Shariff Shamba jijini Dar es Salaam.
Akiwa mkufunzi chuoni hapo, wanafunzi wengi wanamkumbuka kwa ucheshi wake na mwingi wa kuomba msamaha pindi anapochelewa kuingia katika kipindi chake.
Mbali na TSJ, Mzee Tonge aliwahi kuwa mkufunzi Dar es Salaam School of Journalism kilichopo Ilala, Sharrif Shamba.
Pia aliwahi kuhudumu SHIHATA, Idara ya Habari MAELEZO na kwingineko kama mpiga picha.
Uongozi wa DIRAMAKINI BLOG unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa Mzee Tonge kwa kuondokewa na mpendwa wao, Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema. Amen