NA MWANDISHI MAALUM
WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) umeendesha semina elekezi ya kuwajengea uwezo na Kutoa elimu kwa Viongozi wa Wilaya ya Ubungo, Madiwani na Wawakilishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Ubungo kuhusu mfumo mpya wa Kielektroniki wa malipo ya Ushuru wa maegesho ya magari.
Akifungua semina Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Bw. Kheri James ameipongeza TARURA kwa kuandaa semina hiyo na amehaidi kutoa ushirikiano.
Picha mbalimbali zikionesha Viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Ubungo,
Madiwani na Wawakilishi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya
Ubungo wakati TARURA ikiwapa elimu kuhusu mfumo mpya wa Kkelektroniki wa malipo ya ushuru wa
maegesho ya magari.(Picha zote na TARURA).
Ofisi ya Rais ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), TARURA kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango wameboresha mfumo, sasa kumbukumbu namba (Control number) itapatikana ndani ya dakika moja kwa kutumia njia ya Kutolewa Ankara kupitia kwa Mkusanya Ushuru.
Kwa kutumia TeRMIS App (inayopatikana PlayStore), Kwa kutumia GePG App (inayopatikana PlayStore & AppStore), Kwa kutumia simu ya mkononi Piga *152*00# kisha fuata maelekezo na Kwa kutumia Wavuti ya mfumo inayopatikana kwa www.termis.tarura.go.tz.
Pia, TARURA imeboresha eneo la utoaji wa Elimu kwa kuanzisha Dawati la Malalamiko na kuweka namba za simu ambazo ni 0733-149658, 0733–149659 au 0733-149660 na kupitia namba hizi mteja atapiga simu na kutatuliwa changamoto yake. Pia anaweza kuwasilisha lalamiko lake katika Ofisi za TARURA zilizopo karibu yake.
Jinsi ya kulipia maegesho kwa kutumia simu ya mkononi
Piga *152*00#
1. Chagua 4 (Nishati, Madini na Usafiri)
2. Chagua 2 (TARURA)
3. Chagua 1 - Lipia Maegesho
4. Ingiza namba ya chombo cha Moto
5. Utapokea ujumbe mfupi
6. Bonyeza 1 Kuendelea
7. Ingiza namba ya Siri
8. Bonyeza 1 Kuthibitisha malipo ya Serikali.