NA MWANDISHI DIRAMAKINI
MSEMAJI Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Gerson Msigwa amekumbushia moja wapo ya kumbukumbu muhimu katika maisha yake wakati akitekeleza majukumu yake kama mwanahabari mwaka 2013.
"Nimekumbuka mwaka 2013. Hapo ilikuwa tunavuka Mto Ruhuhu ambao ni mpaka wa Wilaya ya Nyasa (Ruvuma) na Ludewa (Njombe).
"Kuvuka hapo ilikuwa lazima Wazee wajulishwe. Yaani hapo nipo kwenye mtumbi nampiga picha Nape Nnauye na ng’ambo ya pili Mzee Abdulrahaman Kinana anaangalia vijana watavuka kweli?.
Mzee Kinana mwenye alivuka kikakamavu mno huku anapiga saluti. Mnaokumbuka ilikuwa ni Operesheni nini vile?.
Mzee Kinana wakati huo alikuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa
huku Nape Nnauye ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Jimbo la Mtama mkoani Lindi akiwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho.