NA MWANDISHI DIRAMAKINI
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es salaam na Lindi pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Angalizo hilo limetolewa leo Novemba 28, 2021 na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ikiwa ni taasisi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba 2 ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutiwa saini tarehe 13 Februari 2019.
TMA ni taasisi mahususi na pekee katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye Mamlaka ya kutoa huduma za Hali ya Hewa ndani ya Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makao Makuu ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania yapo jijini Dar es salaam, aidha mamlaka inatoa huduma zake pia kupitia vituo vyake vilivyopo katika maeneo mbalimnali mikoani.