NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Mkuu wa Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Jokate Mwegelo amechaguliwa kuwania tuzo za kidigitali Tanzania, 2021 kwenye vipengele vinne vya tuzo hizo.
Vipengele vya tuzo hizo ni;
1. Kiongozi bora wa Serikali (Mwanamke) kwenye mitandao ya kijamii
2.Mwanasiasa bora wa kidigitali
3.Mshawishi bora wa mwaka
4.Chaguo bora la watu
>Tunawaomba tumpigie kura Mhe.Jokate Mwengelo kwa kufuata maelekezo haya chini 👇
1. Tembelea 👇
2. Bofya 'Vote Now'
3. Bofya kitufe cha 'Cast Your Vote'
4. Ingiza namba yako ya simu au barua pepe
5. Chagua Digital Governance
6. Pitia vile vipengele vinne ambavyo tumekutajia awali hapo, tafuta jina la Jokate Mwengelo
6. Bonyeza alama ya kujumlisha (+) mara 5 kisha Bonyeza Vote
>ASANTE SANA KWA KURA YAKO🙏🏻
Mheshimiwa Jokate amesema kuwa,mitandao ya kijamii imemsaidia kwenye vitu mbalimbali ikiwemo kufikisha ujumbe kwenye jamii.
“Binafsi mitandao hii imenisaidia sana kufikisha ujumbe na kupata ‘support’ (ushirikiano) ya watu wengi katika kufanikisha malengo na shabaha za serikali sambamba na malengo binafsi ninayojiwekea kama kiongozi katika kuchagiza yale makubwa ya Serikali kwenye nafasi ya uongozi niliyoteuliwa kutumikia. Pia Jokate amewashukuru wote kwa kuonesha ushirikiano kwenye tuzo hizo; “Nitumie fursa hii adhimu kushukuru sana wote walionipendekeza kuwania kwenye vipengele vinne vya tuzo hizi, pia nawapongeza sana waandaaji wa tuzo hizi,”amesema.