Msimamizi wa Ujenzi wa Mradi wa kuzalisha umeme wa maji ya Mto Ijangala, Mhandisi Lydia Malaki (aliyevaa ‘reflector’) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (mwenye fulana ya bluu), hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo wakati wa ziara ya Menejimenti ya REA iliyofanyika Novemba Mosi, 2021 katika Wilaya ya Makete mkoani Njombe. Mradi huo unasimamiwa na KKKT kupitia kampuni ya Nishati Lutheran Associate na imepatiwa ruzuku ya takribani shilingi milioni 400 kutoka REA.
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy (wa tano kutoka kulia waliosimama) na Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Kati, Mhashamu Wilson Sanga (wa nne kutoka kulia - waliosimama), wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi na viongozi wa Kijiji cha Masisiwe wakati wa ziara ya Menejimenti ya REA kutembelea Mradi wa kuzalisha umeme wa maji ya Mto Ijangala uliopo katika kijiji hicho, Wilaya ya Makete mkoani Njombe, Novemba Mosi, 2021. KKKT kupitia kampuni ya Nishati Lutheran Associate imepata ruzuku ya takribani shilingi milioni 400 kutoka REA kwa ajili ya Mradi huo ambao upo katika hatua ya ujenzi. (Picha zote na REA).