VSO yawezesha vijana wenye ulemavu Geita

NA ROBERT KALOKOLA

VIJANA wa kike waliopata mimba na kulazimika kusitisha masomo yao na kushindwa kurudi shule ili kuendelea na masomo pamoja na wenye ulemavu kutoka Wilaya ya Geita mkoani wameanza kunufaika na mafunzo ya ujuzi wa aina mbalimbali ya kuwawezesha kupambana na ukosefu wa ajira ili kujikwamua kiuchumi na kukuza kipato chao.

Mafunzo hayo ya ujuzi kwa vijana hao pamoja walemavu yanatolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo nchini (SIDO) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Kujitolea (VSO) kupitia Mpango wa Kuwezesha Vijana (Youth Economic empowerment-YEE) unaotekelezwa katika Wilaya ya Geita na mwaka 2022 Januari utaanza kwa kunufaisha vijana 35 kutoka Halmashauri mbili ya Geita mji na Geita wilaya.

Ujuzi unaotolewa kwa vijana hao ni pamoja na ushonaji wa nguo,usindikaji wa vyakula mbalimbali,utengenezaji wa sabuni na batiki,ufugaji wa kuku pamoja elimu ya kutunza mazingira ili vijana hao waweze kutunza mazingira hasa kutengeneza mkaa mbadala.
Photunatus Nyundo ambaye ni Mshauri wa Vijana kutoka VSO amesema kuwa, shirika hilo limeamua kuchagua kundi la vijana wa kike waliopata mimba pamoja na walemavu baada ya kubaini kuwa ni moja ya makundi ambayo yanasahaulika kwenye jamii na yanaendelea kushindwa kujikwamua kiuchumi.

Amesema kuwa, mradi huo unatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu na unashirikisha Chama cha Wafanyabiashara Wananwake (TWCC) pamoja na Chama cha Wanasheria wa Mazingira nchini (LEAT) kwa kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) utaanza na vijana 35 ambao 20 ni kutoka Halmashuri ya Wilaya ya Geita na 15 Halmashauri ya mji wa Geita.

Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Geita, Bakari Kitoboli amesema kuwa, shirika hilo litasimamia mafunzo yote kuanzia mwanzo hadi kuhitimu na baada ya hapo watafuatilia mhitimu mmoja mmoja ili kuhakikisha mafunzo hayo yanawanufaisha kwa kuboresha ujuzi wao na kuwaleta maendeleo kwa kuinua uchumi wao na kupunguza utegemezi wa kiuchumi.

Ameongeza kuwa, shirika la SIDO limekuwa likitoa mafunzo ya aina mbalimbali kwa vijana na wajasiriamali kwa kushirikiana na taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali na baada ya mafunzo shirika hilo huwaandalia utambulisho maalum katika taasisi za ubora kama TBS ili bidhaa na huduma wanazotoa ziweze kutambuliwa kisheria na kushindana sokoni.

Bakari Kitoboli ameongeza kuwa, kwa mwaka wa fedha 2019/2020 hadi sasa SIDO Mkoa wa Geita imeishatoa mafunzo ya ujuzi wa aina mbalimbali kwa wajasiriamali zaidi ya miasaba ambao wamefuzi.

Amewataka watu wanaotaka kupata nembo za ubora kutoka mamlaka za udhitibi kuwasiliana na SIDO kwa hatua zaidi ili waweze kupata utambulisho.

Naye Afisa Habari wa VSO, Nicolaus Ambwene amesema ,shirika hilo limeamua kuja na mpango huo wa kuwawezesha vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli tofauti tofauti za ujasiriamali ili waweze kupambana na ukosefu wa ajira na wajiajiri wenyewe.

Ameongeza kuwa, mradi huo wa kuwezesha vijana unatekelezwa katika mikoa Miwili ya Geita na Mkoa wa Mara na utafanya kazi kwa muda wa miaka mitatu kwa kuanza kutoa mafunzo hayo bure kwa vijana 35 kuanzia Januari 2022 ambayo yanahusisha vijana kutoka Halmashauri ya mji wa Geita na Halmashauri ya Wila ya ya Geita.

Ambwene amefafanua kuwa, kazi nyingine ambazo zimefanywa na VSO ni pamoja na kufanya na kuunda kamati za ufuatiliaji wa mapatoo na matumizi hasa kwenye sekta ya madini,kutoa msaada wa kisheria kwa watu 1000,kutoa mafunzo kwa wajasiliamali pamoja na vijana 142 , maigizo ya jukwaani matano yaliyo wafikia watu takribani 2000 na kufanya vikao na mashirika ya kijamii (CBO) kumi na mbili ambapo Geita mjini ni saba na wilaya ni tano.

Samson Jacob na Debora Benard ambao ni wakufunzi waliteuliwa na SIDO kwa ajili ya kufundisha vijana hao ujuzi wa ushonaji kwa muda usiozidi miezi mitatu wamesema kuwa, kazi ya ushonaji nguo ina faida na imewawezesha kujikwamua kiuchumi bila kutegemea kuajiriwa na wameweza kufanya mambo yao ya muhimu kama kujenga nyumba,kusomesha watoto na kununua chakula.

Shirika la VSO linafanya kazi nchi mbalimbali Duniani kwa mfumo wa kujitolea na kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita limeshafikia watu milioni sita katika nchi 33 katika afya jamii ( Health Community) kwa kuamini kuwa jamii ikishikamana na kujitolea inaweza kuondokana na umasikini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news