Wadaiwa sugu NHC kuanza kukabidhi funguo

NA MWANDISHI MAALUM

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) linatarajia kuanza kuwaondoa wapangaji wa nyumba zake ambao ni wadaiwa sugu kuanzia mapema mwezi Desemba 2021.
Baadhi ya Wapangaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Hayupo pichani) wakati wa kikao chake na wapangaji wa Shirika hilo kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na wapangaji wa shirika hilo jijini Mwanza ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi kukagua utekelezaji wa shughuli za sekta ya ardhi na zile za shirika la Nyumba la Taifa pamoja na kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi changamoto za ardhi.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linadai takriban Bilioni 26 Kwa wapangaji wa nyumba zake jambo alilolieleza linachangia kuzorotesha kasi ya utendaji kazi wa shughuli za kila siku za shirika ikiwemo ukarabati

‘’Tutachofanya sasa, yeyote aliyelimbikiza deni na tushampa notisi lakini bado halipi kodi basi zoezi la kumuondoa litafanyika bila hata kumtaarifu upya,’’alisema Dkt.Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao chake na Wapangaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki. Mkuu wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Amina Makilagi akizungumza katika kikao na Wapangaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kilichofanyika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki.

Aliongeza kuwa, oparesheni a kuwaondoa wadaiwa sugu wa nyumba za NHC itaenda sambamba na kuwaondoa wapangaji wote wasio waaminifu waliopangisha nyumba za shirika kwa gharama nafuu huku nao wakipangisha watu wengine kwa gharama kubwa ambapo alikielezea kitendo hicho kuwa ni kuiibia Serikali na halikubaliki kwa kuwa ni kosa kisheria.

Aliwahakikishia wapangaji wa Nyumba za NHC kuwa, Shirika hilo limeanza kufanya ukarabati wa nyumba zake ikiwa ni mpango wake wa miaka mitano na tayari kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni hamsini kimetengwa kwa ajili ya shughuli hiyo
Mmoja wa wapangaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) akiwasilisha kero yake kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa kikao na Wapangaji wa Shirika hili kilichofanyika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza mwishoni mwa wiki. (PICHA ZOTE NA YUSUPH LUDIMO MANISPAA YA ILEMELA).

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi mbali na kupongeza shughuli zinazofanywa na Shirika la Nyumba la Taifa aliliomba shirika hilo kuona namna ya kuzifanyia marekebisho baadhi ya nyumba zake hasa upakaji upya wa rangi baada ya Serikali kuwapanga upya wafanya biashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga maeneo ya miji ili kupendezesha Mji

Naye Meneja wa NHC mkoa wa Mwanza Fadhili Anyegile alisema, kwa mwaka wa 2021/2022 shirika hilo limeweka mikakati ya kuhakikisha linapunguza malimbiko ya madeni ya wapangaji kwa asilimia mia moja, kutoa elimu kwa wapangaji juu utaratibu wa kulipa kodi kwa wakati na kuendelea na zoezi la kufanya matengenezo makubwa na madogo katika nyumba zake ili kuzifanya kuendelea kuwa imara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news