Wadau,watafiti, wanataaluma kufanya Kongamano la Tatu la Utafiti kwa Maendeleo Jumuishi kesho

NA DOREEN ALOYCE

WADAU wa Maendeleo, watafiti na wanataaluma kutoka katika nyanja mbalimbali wanatarajia kufanya kongamano la tatu la utafiti kwa maendeleo jumuishi lengo likiwa ni kujadili kwa pamoja jinsi ya kuboresha maisha ya watanzania na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
Profesa Bernadeta Lillian ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo (Utafiti) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema, kongamano hilo litakalofanyika jijini Dodoma kesho litaleta fursa ya kuwafahamisha wadau kuhusu matokeo ya utafiti katika miradi mabalimbali iliyofanywa na maprofesa, wahadhiri na wanafaunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Aidha, amesema katika kongamano hilo washiriki zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo wanadiplomasia, wabunge, watunga sera na wadau kutoka mashirika yasiokuwa ya kiserikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news