NA HADIJA BAGASHA
IDARA ya Uhamiaji mkoani Tanga imewafikisha mahakamani wahamiaji haramu wapatao 234 raia wa Ethiopia walioingia nchini kinyume cha sheria kwa nyakati tofauti kuanzia Septemba mwaka huu huku wengine 600 wakiwa katika Gereza Kuu la Maweni.
Sanjari na wahamiaji hao kukamatwa na kufikishwa mahakamani, wengine zaidi ya 600 wapo katika gereza Kuu la Maweni mkoani Tanga, wakitumikia vifungo na wengine wakisubiri mashauri ya kesi zao zilizopo mahakamani.
Amesema, katika wahamiaji hao wapo pia Watanzania tisa ambao walikutwa wakiwasafirisha kwa kutumia usafiri wa pikipiki tano ambazo zinashikiliwa na idara hiyo na endapo watatiwa hatiani na mahakama, pikipiki hizo zitataifishwa na serikali.
Kamanda huyo amesema, wahamiaji hao wamefikishwa mahakamani nusu yao na wengine watafikishwa siku inayofuatwa kutokana na idadi yao kubwa.
Amesema, kwa upande wa Watanzania endapo watapatikana na makosa adhabu yao ni kifungo cha miaka 20 jela au kulipa faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja.