NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amewashauri wakulima katika Kata ya Gua iliyopo wilayani Songwe mkoani hapa kulima zao la pilipili ikiwemo kufuga nyuki pembezoni mwa vijiji vinavyopakana na hifadhi ili kuepuka hasara inayotokana na mazao yao kuharibiwa na tembo.
RC Mgumba ameyasema hayo baada ya wananchi wa kata hiyo kutoa malalamiko kwake, baada ya kufika katika kata hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tatu wilayani humo kwa kengo la kusikiliza kero.
Amesema, wakulima katika vijiji vya kata hiyo ambayo imepakana na Hifadhi ya Wanyamapori ya Piti Lukwati wanatakiwa kulima zao la pilipili.
Sambamba na kufuga nyuki kama njia bora ya kakabiliana na changamoto ya tembo kuvamia mashamba yao na kuharibu mazazo.
"Nashauri kwamba kila mkulima ahakikishe anapanda zao la pilipili au kufuga nyuki kuzunguka shamba lake na hapo tutakuwa tumewadhibiti wanyama hawa katika njia bora zaidi,"amesema RC Mgumba.
Aidha, katika mkutano huo wananchi wa kata hiyo waliomba serikali kuona uwezekaoa wa kuwapatia fidia baada ya tembo wa hifadhi ya Piti Lukwati kuharibu zaidi ya ekari 70 za mashamba ya mahindi na tumbaku.
Pia wakulima hao waliiomba Serikali kuwasaidia namna ya kuwadhibiti tembo kwa kuwa kitendo cha wanyama hao kuvamia mashamba yao kila mwaka huwasababishia hasara kubwa.
Ofisa Wanyamapiri wa Hifadhi ya Piti Lukwati, Brayani Nyella alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la tembo kuvamia na kuharibu mashamba ya wananchi na kwamba hali hiyo inatokana na ongezeko la wanyama hao katika hifadhi hiyo.
Nyela alimetoa wito kwa wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo kutoa taarifa haraka pindi wanapovamiwa na wanyama hao ili waweze kupata msaada.
Tags
Habari