Watanzania wapewa mbinu za kupaisha uchumi

NA DOREEN ALOYCE

IMEELEZWA kuwa Tanzania ili ifike kwenye uchumi wa kati Watanzania wametakiwa kufanya kazi kwa bidii kwa kujibidisha na fursa mbalimbali zinazowazunguka jambo ambalo litasaidia kuleta ufanisi mkubwa kwa Taifa .
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma Aziza Mumba ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua semina ya wajasiliamali wadogo wanaojihusisha na uzalishaji wa mvinyo Mkoani Dodoma yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Shirika la SIDO.

Mumba amesema kuwa, Serikali inaaendelea na mnyororo wa thamani hasa katika zao hilo la zabibu, hivyo wajasiriamali wanapaswa kutokukata tamaa ili waweze kukuza uchumi wao na Taifa.

Amesema kwa, hapa Dodoma zao la zabibu ni la kimkakati na lengo ni wakulima wauze bidhaa safi huku Serikali na wawekezaji wakiangalia namna ya kuanzisha viwanda zaidi vya kusindika zabibu ziwe juice na kwamba tayari Kuna viwanda vidogo 18 na vya kati vitatu.

"Nashukuru TBS kwa kufanya haya mafunzo kuwapatia ujuzi na kuwajengea uwezo ili wawe jasiri katika usindikaji wa zabibu jambo ambalo litawasaidia sana katika kuongeza kipato chao na kupata soko kubwa ndani na nje ya nchi,"amesema Mumba.
Amezitaka halmashauri zote Mkoa wa Dodoma kuendelea kutoa ushirikiano kwa TBS wanapoendelea kutoa bidhaa zenye viwango.

Nae Meneja wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati,Nickonia Mwabuka amesema kuwaTBS imeandaa mafunzo haya kwa kushirikiana na SIDO lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo ili waweze kuzalisha bidhaa zenye ubora na usalama hatimaye kujikwamua kiuchumi.

"TBS inasaidia kupima bidhaa hizi ili ziweze kuwa na soko za Kimataifa na mpaka Sasa Wasindikaji 15 wamefaidikia na mfumo huu na kupitia mafunzo haya yatafanikiwa kwa Kiasi kikubwa,"amesema Mwabuka.
Kwa upande wao wajasiriamali walioshiriki mafunzo hayo wamesema kwamba, kwao ni fursa kubwa bapo wataenda kujifunza namna ya kuboresha bidhaa zao zinazotokana na zabibu jambo ambalo litasaidia kupata masoko na kujulikana ndani na nje ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news