Waungana kwa wiki mbili kumuombea Rais Samia

NA ROTARY HAULE

WAUMINI wa makanisa ya Kipentekoste yaliyopo Kibaha Mkoani Pwani wameungana kwa pamoja kwa ajili ya kufanya maombi ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ili aweze kuendelea vyema katika kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia Watanzania.

Maombi hayo yamefanyika katika Kanisa la Harvest Gospel Pentecostal Church lililopo katika Mtaa wa Mwanalugali Kibaha Mjini chini ya usimamizi wa askofu Emmanuel Mhina.

Akisoma risala ya kufunga maombi hayo kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibaha Mjini SP Ernest Shalua ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Mwangalizi wa Mkuu wa Makanisa ya Harvest Gospel Pentecostal Church Askofu Emmanuel Mhina,amesema kuwa maombi hayo yamefanyika kwa muda wa wiki mbili lakini yatakuwa endelevu.
Mhina,amesema kuwa lengo la maombi hayo ni kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ili haweze kuendelea vyema kutekeleza majukumu yake ya kuhudumia Watanzania.

Amesema,Rais Samia amepokea kiti cha Urais katika mazingira magumu lakini hatahivyo amekuwa akifanyakazi yake vizuri na nchi imetulia kwahiyo wameona ni waungane baadhi ya makanisa kumuombea Rais na Taifa kwa ujumla.

"Tumeungana baadhi ya makanisa ya Kipentekoste na tumeweka kambi ya wiki mbili hapa kanisani kwa ajili ya kumuombea Rais wetu ili hapate afya njema itakayomsaidia kuendelea kuwahudumia wananchi wake na tunashukuru toka achukue kiti cha Urais amekuwa akifanyakazi vizuri sana na nchi imetulia," alisema askofu Mhina

Aidha,Mhina amesema mbali na kumuombea Rais lakini pia maombi hayo yameelekezwa katika kuwaombea viongozi wengine na mihimili inayomsaidia Rais kufikia malengo ya kutekeleza majukumu hayo.

Amesema kuwa,maombi hayo yamegusa viongozi wa Serikali,Bunge,Mahakama na maombi ya kupinga masuala ya ugaidi huku akipongeza juhudi za vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kulinda amani ya Taifa.

"Tunamshukuru Mungu kupitia vyombo vya Ulinzi na Usalama vilisimama vyema katika kudumisha usalama tofauti na nchi nyingine hadi tulipompata Rais mpya Mama Samia Suluhu Hassan lakini lazima tumuombee Rais wetu kwakuwa alipoketi kiti hicho kwa ughafla pasipo kutarajia na akakubali kwa moyo kubeba jukumu zito la Kitaifa la kuongoza nchi," amesema Mhina.

Kwa upande wake Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibaha Mjini, SP Ernest Shalua amewashukuru waumini hao kwa hatua waliyochukua kwakuwa inalengo la kuleta amani na kudumisha usalama wa nchi.
Shalua,amesema Mungu ametupa Rais Samia Suluhu Hassan lazima tumuombee kwakuwa anafanyakazi kubwa yenye kuleta faraja licha ya kuondokewa kiongozi mkubwa John Magufuli.

"Kanisa hili la Mwanalugali limefanya jambo kubwa na jema sana la kufanya maombi ya kumuombea Rais Samia na Taifa na mimi naomba maombi haya yaendelee na tuombe sana amani kwakuwa amani ikiwepo uchumi utakuwa mzuri,Madini yetu yatabaki ,mali zetu zitabaki kwa ajili ya kusaidia Watanzania,"amesema Shalua.

Hata hivyo,Shalua amesema Rais Samia ni shupavu na amekuwa akitekeleza majukumu yake bila mashaka na bila uoga hivyo lazima makanisa yaendelee kusimama kwa ajili ya kuombea Taifa na viongozi wake kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news