Waziri Mchengerwa akoleza moto vita dhidi ya rushwa, ubadhirifu

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka viongozi wote kutumia nasaha za waasisi wa Taifa letu katika kupambana na rusha ukiwemo ubadhirifu wa mali za umma.

Mheshimiwa Waziri Mchengerwa amesema hayo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021 wa Viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) uliofanyika Novemba 25, 2021 jijini Dodoma.

Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021 wa Viongozi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) uliofunguliwa rasmi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa umefanyika kwa siku tatu kuanzia Novemba 25 hadi 27, 2021.

Pia alitumia nafasi hiyo kueleza wazi kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anaamini kuwa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) itamsaidia kujenga taifa ambalo wananchi anaowaongoza watanufaika na uwepo wa rasilimaliwatu na rasilimali za umma zilizopo pasipo kuombwa wala kutoa rushwa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news