NA MWANDISHI MAALUM
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kuipatia vitendea kazi (kompyuta) Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ili kuharakisha shughuli za usuluhishi wa migogoro ya kikazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (wapili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Bw. Shanes Nungu (wapili kushoto) moja kati ya kompyuta 10 zilizotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Novemba 29, 2021 jijini Mbeya. Wanaoshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. Kaspar Muya (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma.
Pongezi hizo zimetolewa na Mhe. Waziri Jenista wakati akikabidhi kompyuta 10 kwa Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw.Shanes Nungu katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za Mfumo wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Mbeya Novemba 29, 2021.
“Tunashuhudia hapa Workers Compensation Fund (Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi) unakwenda kufanya kazi nzuri ya kuiwezesha CMA ili itekeleze majukumu yake sawasawa jambo hili ni zuri sana,"amefafanua Mhe. Waziri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea computer kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma ambazo zilitolewa na Mfuko kuisapoti CMA.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza kwenye hafla hiyo.
"Kipekee napenda kuwashukuru sana sana wakuu wote na viongozi wa taasisi zote Dkt. John Mduma Mkurugenzi Mkuu wa WCF na kaka yangu Nungu Mkurugenzi Mkuu wa CMA kwa kuona umuhimu wa kufanya kazi kama serikali moja, ninyi wote mko chini ya umbrella (mwamvuli) mmoja, ili kuhakikisha kwamba mmoja anapogundua changamoto ya mwenzake anaamua kusimama naye na kuweza kumsaidia,"amesisitiza Mhe. Waziri Jenista Mhagama.
Akieleza zaidi, Mhe. Waziri alisema Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa ukifanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yake tangu uanzishwe miaka sita iliyopita, sheria iliyokuwepo kabla ya kupata uhuru, mfanyakazi alikuwa akiumia analipwa shilingi 108,000 haijalishi awe amepata ulemavu wa aina gani malipo ya fidia yalikuwa ni flat rate.
“Mwaka 2008 Sheria ilifanyiwa marekebisho ambapo mwaka 2015 tuliunda Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ambao umechukua jukumu la Fidia, kuhangaika na magonjwa na madhara yatokanayo na kazi kutoka kwa waajiri na kuwekwa kwenye Mfumo maalum na sasa uko kwenye Mfuko wa WCF,"amebainisha.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Bw. Kaspar Muya, akimkaribisha Mhe. Waziri.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akitoa neno la utangulizi.
Alisema katika muktadha huo huo wa kuhakikisha serikali inayagawa majukumu kiutendaji na kisheria ilianzisha CMA ili taasisi hii ishughulike na masuala ya usuluhishi na uamuzi inapotekea migogoro ndani ya maeneo ya kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt.John Mduma alisema, makabidhiano hayo ya computer ni utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama aliyetaka taasisi hizo zifanye kazi kama ndugu.
“Kwa kufanya kazi kwa pamoja ndipo tunaweza kufikia malengo yetu kama taasisi lakini kwa pamoja kama ofisi yako Mheshimiwa Waziri, tunatambua kwamba mmoja wetu kama atakimbia mbio na uwezo wake alionao na akawaacha ndugu zake nyuma “hatatoboa yeye peke yake,"amesema Dkt. Mduma.
Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw.Shanes Nungu, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko huo, Dkt. Abdulsalaam Omar pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano ya Umma, WCF, Bi. Laura Kunenge, wakati wa hafla hiyo.
Mfawidhi wa CMA jijini Mbeya, Bw. Mwangata Makawa akitoa neno la shukrani.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa CMA.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Idara ya Kazi, Mbeya.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa OSHA.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSSSF.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NSSF.
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa WCF.Naye Mkurugenzi Mkuu wa CMA, Bw. Shanes Nungu alimshukuru Waziri Jenista kwa maono yake na kuwezesha CMA kupata msada huo wa kompyuta.
“Mheshimiwa Waziri nakumbuka ulisema nyie watoto sita kwanza shikamaneni halafu saidianeni na agizo lako limezaa matunda, sio mara ya kwanza kwa WCF kutusaidia mara ya kwanza walitusaidia computer kumi ambazo zilisaidia kutatua malalamiko ya wananchi kucheleweshewa hukumu zao kupungu,” alishukuru Bw. Nungu.
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge) Bw. Kspar Muya, wakurugenzi wa WCFna CMA pamoja na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo ni NSSF, PSSSF, OSHA na Idara ya Kazi.