Waziri Ummy:Muwe tayari kufanya kazi halmashauri za pembezoni

NA NTEGHENJWA HOSSEAH, OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) amesema, wanafunzi wanaomaliza katika Chuo cha Serikali za Mitaa wawe tayari kufanya kazi kwenye halmashauri za pembezoni mara watakapopata ajira kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Waziri Ummy ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye Mahafali ya 13 ya Chuo cha Serikali za Mitaa-Hombolo jijini Dodoma.

Amesema, Mamlaka za Serikali za Mitaa zitaendelea kuajiri wataalam wanaohitimu katika chuo hicho kwa kuwa wamepikwa kutumika vyema kwenye Serikali za Mitaa.
"Sasa mnapopata ajira zetu muwe tayari kwenda kufanya kazi kwenye halmashauri za pembezoni (vijijini) na sio mkishapata tu mnaanza kuomba uhamisho kurudi mjini.

“Watu wa kijijini pia wanahitaji huduma zetu, hivyo watumishi wanahitajika kwenda kufanya kazi maeneo hayo na sio kunga’ang’ania kubakia mjini wakati wote, kila mtu anataka Dodoma Jiji, Kinondoni, Arusha Jiji, Mwana Jiji nani akae Mpimbwe, Uvinza, Kilindi, Rufiji,” alihoji Waziri.
"Ni kweli hata uhamisho nimesitisha na itaendelea hivyo mpaka tutakapofanya msawazo wa watumishi lazima ningalie kwa nini Ukerewe kuna walimu 100 wakati Kinondoni kuna walimu 2,000 tutaangalia mahitaji na waliopo ili kufanya maamuzi sahihi wakati wa kuhamisha,"ameongeza.

Akizungumza katika Mahafali hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Prof. Joseph Kuzilwa ameiomba Serikali kuwezesha ujenzi wa barabara ya Ihumwa - Hombolo kwa kiwango cha lami ili kuweza kufika kiurahisi chuoni hapo tofauti na sasa ambavyo miundombinu hairidhishi.
Naye Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Hombolo Dkt. Mpamile Madale amesema chuo hicho kinakua siku hadi siku na kuongeza udahili na wanafunzi waliohitimu mwaka 2021 ni 6021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news